Pata taarifa kuu

Gambia yawarejesha makwao raia wake 40 kutoka Tunisia

Gambia imewarejesha nyumbani raia wake 40 kutoka Tunisia usiku wa Alhamisi kuamkia Ijumaa, siku moja baada ya operesheni sawia na kundi jingine la wahamiaji waliokwama kwenye barabara ya kuelekea uhamishoni nchini Libya, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ametangaza siku ya Ijumaa Julai 28.

Wahamiaji wa Kiafrika wanasubiri treni katika jaribio la kukimbia mmachafuko ya hivi karibuni huko Sfax, Tunisia, Julai 5, 2023.
Wahamiaji wa Kiafrika wanasubiri treni katika jaribio la kukimbia mmachafuko ya hivi karibuni huko Sfax, Tunisia, Julai 5, 2023. © AFP / HOUSSEM ZOUARI
Matangazo ya kibiashara

Hali imekuwa ngumu sana kwa wahamiaji nchini Tunisia tangu rais Kais Saied, ambaye alichukua mamlaka kamili mnamo Julai 2021, kushutumu wahamiaji haramu mnamo Februari 21, akimaanisha "makundi ya wahamiaji kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara" ambao walikuja, kulingana na rais huyo, " kubadilisha muundo wa raia" wa Tunisia. Hotuba za waziwazi za chuki dhidi ya wageni zimeenea nchini humo.

Kufuatia makabilinao yaliyogharimu maisha ya Mtunisia mmoja mnamo Julai 3, mamia ya wahamiaji wa Kiafrika walifukuzwa kutoka Sfax, mji wa pili wa Tunisia na ambao mwaka huu umekuwa kitovu kikuu cha kuhama kwa wahamiaji haramu kwenda Ulaya. Kisha walichukuliwa na mamlaka, kulingana na mashirika yasiyo ya kiserikali, na kupelekwa katika maeneo yasiyofaa karibu na Libya upande wa mashariki na Algeria upande wa magharibi. Bila maji, chakula au malazi katika joto zaidi ya nyuzi 40, wengi walikufa, shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Rights Watch limesema.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotumwa siku kadhaa baada ya tukio hili, serikali ya Gambia ilisema inajitahidi kuwaondoa raia wake waliopo katika nchi za Afrika Kaskazini.

Wahamiaji hao, ambao walirejeshwa nchini Gambia kwa hiari, waliondoka Tunisia siku ya Alhamisi jioni na kufika katika mji mkuu wa Banjul mwendo wa saa nane usiku kwa saa za Gambia, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ameongeza. Safari ya ndege ya kuwarejesha wahamiaji hao iliandaliwa na serikali ya Gambia, kwa ushirikiano na Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji.

Siku ya Jumatano, nchi za Afrika Magharibi ziliwarejesha makwao raia 87 kutoka Libya, msemaji huyo amesema. Mapema mwaka huu, mataifa ya Afrika Magharibi huko Burkina Faso, Guinea, Côte d'Ivoire, Mali na Senegal yaliwarudisha mamia ya raia wao kutoka Tunisia.

Kati ya Juni 21 na Julai 4, Gambia iliwarejesha makwao karibu raia wake 300 waliozuiliwa wakiwa njiani kuelekea uhamishoni, nusu yao wakiwa wamekwama nchini Libya. Wengine walinaswa kwenye boti katika maji ya Senegal, Mauritania na Morocco. Senegal iliwarejesha nyumbani raia wake 50 kutoka Morocco siku ya Jumatano.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.