Pata taarifa kuu
USALAMA-HAKI

Wahamiaji wa Kiafrika wafukuzwa kutoka Sfax baada ya kifo cha Mtunisia

Makumi ya wahamiaji wa Kiafrika wamefukuzwa katika mji wa Sfax nchini Tunisia ambao umekumbwa na ghasia usiku mwingine baada ya kifo cha mkazi mmoja katika mapigano, kulingana na ushuhuda na picha zilizorushwa mtandaoni.

Vijana wa Tunisia wakichoma matairi baada ya mazishi ya kijana aliyedungwa kisu hadi kufa wakati wa makabiliano na wahamiaji wa Kusini mwa jangwa la Sahara, huko Sfax, Julai 4, 2023.
Vijana wa Tunisia wakichoma matairi baada ya mazishi ya kijana aliyedungwa kisu hadi kufa wakati wa makabiliano na wahamiaji wa Kusini mwa jangwa la Sahara, huko Sfax, Julai 4, 2023. © Lilia Blaise / RFI
Matangazo ya kibiashara

Katika vitongoji kadhaa vya jiji hili kubwa katikati mwa mashariki mwa Tunisia, mamia ya wakaazi walikusanyika mitaani usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano wakitaka wahamiaji wote haramu kuondoka mara moja, kulingana na mwandishi wa shirika la habari la AFP.

Baadhi ya watu walifunga barabara na kuchoma moto matairi kuelezea hasira zao baada ya mkazi mmoja mwenye umri wa miaka 41 kuuawa kwa kuchomwa kisu katika makabiliano na wahamiaji kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Katika video zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii, maafisa wa polisi wanaweza kuonekana wakiwakimbiza makumi ya wahamiaji kutoka kwa nyumba zao huku wakishangilia wakaazi wa jiji, kabla ya kuwapakia kwenye magari ya polisi. Video zingine zimeonyesha wahamiaji wakiwa wamelazwa chini, mikono juu ya vichwa vyao, wakiwa wamezungukwa na wakazi wakiwa na fimbo wakisubiri kuwasili kwa polisi.

Katika ukurasa wa Facebook wa kundi la Sayeb Trottoir linalojitolea kwa suala la uhamiaji haramu, Lazhar Neji, anayefanya kazi katika chumba cha dharura cha hospitali huko Sfax, anasema alisikitishwa "usiku wa kinyama (...) wa umwagaji damu unatia uoga". Kulingana mfanyakazi huo, hospitali hiyo ilipokea kati ya wahamiaji 30 hadi 40, wakiwemo wanawake na watoto. “Wengine walirushwa kutoka kwenye kuta, wengine walishambuliwa kwa mapanga,” amesema.

Wahamiaji kadhaa waliletwa na polisi kwenye eneo la Maonyesho ya Sfax wakati wakisubiri kuhamishiwa mahali pengine, Romdane Ben Amor, mkuu wa Jukwaa la Haki za Kiuchumi na Kijamii (FTDES), shirika lisilo la kiserikali linalofuatlia masuala ya uhamiaji, ameliambia shirika la habari la AFP.

Kulingana naye, wahamiaji wengine walipelekwa katika eneo karibu na mpaka wa Libya. Hakuweza kutaja jumla ya idadi ya wahamiaji waliofukuzwa kutoka Sfax.

Makumi ya wahamiaji wengine wamekimbilia kituo cha reli cha Sfax kuchukua treni hadi miji mingine ya Tunisia, amebainisha mpiga picha wa AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.