Pata taarifa kuu

EU yatafuta makubaliano juu ya wahamiaji na Tunis

Wiki mbili baada ya mojawapo ya ajali mbaya zaidi ya boti ya wahamiaji katika bahari ya Mediterania, viongozi wa Ulaya wanajadili Alhamisi mjini Brussels kuhusu ukamilishaji mgumu wa makubaliano na Tunisia yanayonuiwa kuzuia vivuko wanavyotumia wahamiaji kujaribu kuingia Ulaya na kupambana dhidi ya wasafirishaji haramu.

Njia ya wahamaji inayounganisha Afrika Kaskazini na Italia ndiyo hatari zaidi duniani: zaidi ya vifo 20,000 tangu 2014 vimeripotiwa.
Njia ya wahamaji inayounganisha Afrika Kaskazini na Italia ndiyo hatari zaidi duniani: zaidi ya vifo 20,000 tangu 2014 vimeripotiwa. © Fethi Belaid / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Ulaya ilitarajia kuhitimisha kabla ya mkutano huu wa kilele wa EU mkataba wa maelewano na Tunis kutekeleza "ushirikiano wa kimataifa" ikiwa ni pamoja na kipengele cha uhamiaji. Kwa lengo la kupanua aina hii ya ushirikiano kwa nchi nyingine katika eneo la Mediterania, kama vile Misri. Lakini majadiliano na Tunis, muhimu, hayakuweza kufanikiwa kwa wakati, na yataanza tena siku ya Jumatatu, baada ya Sikukuu ya Waislamu ya Eid al-Adha.

Ushirikiano huo, ambao pia unajumuisha kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na ushirikiano katika nishati ya kijani, unaambatana na msaada wa kifedha wa zaidi ya euro bilioni moja. Ilitangazwa mnamo Juni 11 wakati wa ziara ya rais wa Tume, Ursula von der Leyen huko Tunis, akiambatana na mkuu wa serikali ya Italia, Giorgia Meloni, na mwenzake wa Uholanzi, Mark Rutte. Hata hivyo, inaibua wasiwasi wa baadhi ya nchi wanachama kwa sababu ya msimamo wa rais Kais Saied.

Msaada huo wa Ulaya kwa kiasi fulani unahusishwa na kutoa mkopo wa dola bilioni 2 kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), mkopo unaojadiliwa kwa sasa, na masharti yameambatanishwa. Lakini tangu ziara ya watatu hao, Rais Saied amekuwa akirudia kusema kuwa Tunisia haitakuwa "mlinzi wa mpaka" wa Ulaya na haitasalimu amri kwa kile anachoelezea kama "maelekezo" ya IMF.

Mark Rutte, hata hivyo, alikuwa na matumaini. "Inachukua muda mrefu kidogo," lakini "majadiliano yanaendelea. Natarajia matokeo mazuri," amesema. Ili kuzuia kuvuka, Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis pia ametoa wito wa kuanzisha ushirikiano na Libya "sawa" na makubaliano ya uhamiaji yaliyotiwa saini na Uturuki mnamo mwaka 2016.

Meli, rada na kamera

Kwa undani, msaada wa Ulaya uliotangazwa kwa Tunisia ni pamoja na mkopo wa hadi euro milioni 900, lakini pia msaada wa kibajeti wa euro milioni 150 na kifurushi cha euro milioni 105 kwa usimamizi wa uhamiaji kwa mwaka 2023.

EU inapanga kupeleka meli, rada za kuhamishwa, kamera na magari nchiniTunisia ifikapo majira ya joto ili kuisaidia kuimarisha udhibiti wa mipaka yake ya baharini na nchi kavu. Kuongezeka kwa ushirikiano wa polisi na mahakama imepangwa kupambana na mitandao ya magendo.

Mkataba huo pia unalenga kurejea kwa urahisi nchini kwa raia wa Tunisia wa waishio ugenini ambao wako katika hali isiyo ya kawaida katika nchi za EU. EU pia inafadhili urejeshaji wa "hiari" wa wahamiaji kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahaŕa kutoka Tunisia hadi nchi zao za asili: Marejesho 407 yamefadhiliwa kwa njia hii tangu mwanzoni mwa mwaka, kulingana na Tume ya Ulaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.