Pata taarifa kuu

Tunisia: Idadi ya waliofariki kutokana na kuzama kwa boti ya wahamiaji yafikia 32

Idadi ya waliofariki baada ya boti ya wahamiaji kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara kuzama katika bahari ya Mediterania, ajali ya boti iliyotokea Jumanne wiki hii karibu na Tunisia imeongezeka hadi 32 baada ya miili mipya nane kupatikana, walinzi wa pwani ya Tunisia wametangaza siku ya Ijumaa.

Maiti zilizofunikwa za wahamiaji zimepigwa picha katika bandari ya Sfax, katikati mwa Tunisia, Alhamisi, Desemba 24, 2020. Takriban wahamiaji 20 wa Kiafrika walipatikana wakiwa wamekufa Alhamisi baada ya boti yao kuzama katika Bahari ya Mediterania walipokuwa wakijaribu kuingia Ulaya, mamlaka ya Tunisia imesema. . Boti za walinzi wa pwani na wavuvi wa eneo hilo walipata na kuokota miili hiyo kwenye maji karibu na mji wa pwani wa Sfax katikati mwa Tunisia.
Maiti zilizofunikwa za wahamiaji zimepigwa picha katika bandari ya Sfax, katikati mwa Tunisia, Alhamisi, Desemba 24, 2020. Takriban wahamiaji 20 wa Kiafrika walipatikana wakiwa wamekufa Alhamisi baada ya boti yao kuzama katika Bahari ya Mediterania walipokuwa wakijaribu kuingia Ulaya, mamlaka ya Tunisia imesema. . Boti za walinzi wa pwani na wavuvi wa eneo hilo walipata na kuokota miili hiyo kwenye maji karibu na mji wa pwani wa Sfax katikati mwa Tunisia. AP - Houssem Zouari
Matangazo ya kibiashara

Siku moja baada ya kuzama kwa meli hii katika bahari ya Mediterania karibu na Sfax katikati mwa mashariki mwa Tunisia, walinzi wa pwani waliripoti vifo vya watu kumi kabla ya kurekebisha tena idadi ya wahamiaji siku ya Alhamisi baada ya kupata miili 14 mipya ya wahamiaji pamoja na ile ya "nahodha" wa boti hiyo, raia wa Tunisia.

Siku ya Ijumaa, msemaji wa kikos ca walinzi wa kitaifa, mamlaka inayohusika na ulinzi wa Pwani, ametangaza kwamba walinzi hao walipata miili nane mipya ya wahamiaji wakati wa operesheni ya kuwatafuta, na kufanya idadi ya raia wa nchi kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara kufikia 32 ambao waliangamia katika mkasa huu.

Makumi ya wahamiaji kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wameangamia katika wiki za hivi karibuni baada ya boti zilizokuwa zikiwasafirisha kinyemela kwenda Ulaya kuzama nje ya Tunisia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.