Pata taarifa kuu

Uhamiaji haramu: klabu ya soka ya Tunisia yajikuta haina wachezaji

Klabu ya soka inayoshiriki ligi ya daraja la nne ya michuano ya Tunisia imesitisha shughuli zake baada ya wachezaji wake 30 kuhamia Ulaya kinyume cha sheria, Mtendaji mkuu wa klabu hiyo ametangaza.

Takriban wahamiaji 280 waliokolewa na Walinzi wa Pwani ya Italia baada ya kugunduliwa karibu na eneo la Lampedusa, Italia, Januari 24, 2022.
Takriban wahamiaji 280 waliokolewa na Walinzi wa Pwani ya Italia baada ya kugunduliwa karibu na eneo la Lampedusa, Italia, Januari 24, 2022. AP - Pau de la Calle
Matangazo ya kibiashara

Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, si chini ya wachezaji 32 kutoka klabu ya wachezaji mahiri ya Ghardimaou wamehamia Ulaya kinyume cha sheria, Mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Jamil Meftahi, ameliambia AFP.

"Tumeamua kusitisha shughuli na kusimamisha mechi siku 20 zilizopita," ameongeza. Afisa huyo amehusisha kutoroka kwa wachezaji na "ukosefu wa rasilimali za kifedha" wa klabu na wachezaji. "Hatuwezi kununua vifaa, jezi na viatu vya michezo" na wachezaji "hawanufaiki na ruzuku wanayopata kwa klabu hii".

Kulingana na Jamil Meftahi, wachezaji wengi, wenye umri wa miaka 17 hadi 22, waliingia Ulaya "ama kwa njia ya baharini au kwa kupitia Serbia (nchi ambayo raia wa Tunisia walikuwa wakiingia bila visa hadi hivi karibuni) na kisha kuvuka mipaka kwa nchi nyingine kinyume cha sheria" .

Kusimamishwa kwa shughuli za klabu kutaendelea "hadi tutakapopata suluhu na Shirikisho la Soka la Tunisia", ameongeza Meftahi. Ghardimaou ni mji wa mpaka na Algeria ulioko kaskazini-magharibi mwa nchi, eneo lililotengwa ambalo linategemea sana kilimo.

Katika miaka ya hivi karibuni, uhamiaji haramu wa wanariadha wa Tunisia umeongezeka mara kwa mara. Katikati ya mwezi Februari, klabu ya Avenir Sportif huko Rejiche ilitangaza kwamba kipa wake mbadala, Khalil Zaouli, mwenye umri wa miaka 19, alihamia Italia kinyume cha sheria, kutokana na "shida za kifedha za klabu".

Tunisia, baadhi ya sehemu za ukanda wa pwani ambazo ziko chini ya kilomita 150 kutoka kisiwa cha Italia cha Lampedusa, mara kwa mara hurekodi watu visa vya watu kuingia Ulaya, hususan Italia, hasa kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Katika miaka ya hivi karibuni, maelfu ya raia wa Tunisia ambao wanakabiliwa na hali ya kiuchumi na kijamii ambayo imezorota zaidi tangu mapinduzi ya Rais Kais Saied mwaka mmoja na nusu uliopita,  pia wameondoka nchini kinyume cha sheria kwa njia ya bahari.Wizara ya Mambo ya Ndani ya Italia inasema zaidi ya wahamiaji 14,000 wametua nchini humo tangu mwanzoni mwa mwaka, ikilinganishwa na zaidi ya 5,300 katika kipindi kama hicho mwaka jana na 4,300 mnamo mwaka 2021.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.