Pata taarifa kuu

EU yatafuta makubaliano juu ya wahamiaji na Tunis

Wiki mbili baada ya mojawapo ya ajali mbaya zaidi ya boti ya wahamiaji katika bahari ya Mediterania, viongozi wa Ulaya wanajadili Alhamisi mjini Brussels kuhusu ukamilishaji mgumu wa makubaliano na Tunisia, mkutano unaonuiwa kuzuia wanakopitia wahamiaji na kupambana dhidi ya wasafirishaji haramu.

Wahamiaji kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wanapatikana karibu na jiji la Tunisia la Sfax, katika Bahari ya Mediterania, na mamlaka ya Tunisia wakati wakijaribu kufanya safari zao kwa siri kuelekea pwani ya Italia, Oktoba 4, 2022.
Wahamiaji kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wanapatikana karibu na jiji la Tunisia la Sfax, katika Bahari ya Mediterania, na mamlaka ya Tunisia wakati wakijaribu kufanya safari zao kwa siri kuelekea pwani ya Italia, Oktoba 4, 2022. © Fethi Belaid / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Ulaya ilitarajia kuhitimisha kabla ya mkutano huu wa kilele wa EU, mkataba wa maelewano na Tunis ili kutekeleza "ushirikiano wa kimataifa" ikiwa ni pamoja na kipengele cha uhamiaji. Kwa lengo la kupanua aina hii ya ushirikiano kwa nchi nyingine katika eneo la Mediterania, kama vile Misri. Lakini majadiliano na Tunis, muhimu, hayakuweza kufanikiwa kwa wakati, na lazima yaanze tena Jumatatu, baada ya sikukuu ya Waislamu ya Eid al-Adha.

Ushirikiano huo, ambao pia unajumuisha kuimarisha uhusiano wa kiuchumi na kibiashara na ushirikiano katika nishati ya kijani, unaambatana na msaada wa kifedha wa zaidi ya euro bilioni moja. Ilitangazwa mnamo Juni 11 wakati wa ziara ya Rais wa Tume, Ursula von der Leyen huko Tunis, akifuatana na mkuu wa serikali ya Italia, Giorgia Meloni, na mwenzake wa Uholanzi, Mark Rutte. Hata hivyo, inaibua wasiwasi wa baadhi ya nchi wanachama kwa sababu hatua za rais Kais Saied.

Msaada huo wa Ulaya kwa kiasi fulani unahusishwa na kutolewa kwa Shirika la Fedha Duniani (IMF) mkopo wa dola bilioni 2 unaojadiliwa kwa sasa, na masharti yameambatanishwa. Lakini tangu ziara ya watatu hao, Rais Saied amekuwa akirudia kusema kwamba Tunisia haitakuwa "walinzi wa mpaka" wa Ulaya na haitasalimu amri kwa kile anachoelezea kama "maelekezo" ya IMF.

Mark Rutte, hata hivyo, alikuwa na matumaini. "Inachukua muda mrefu zaidi," lakini "majadiliano yanaendelea. Natarajia matokeo yatakuwa mazuri," alisema. Ili kuzuia kuvuka, Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis pia alitoa wito wa kuanzisha ushirikiano na Libya "sawa" na makubaliano ya uhamiaji yaliyotiwa saini na Uturuki mnamo mwaka 2016.

Boti, rada na kamera

Kwa undani, msaada wa Ulaya uliotangazwa kwa Tunisia ni pamoja na mkopo wa hadi euro milioni 900, lakini pia msaada wa kibajeti wa euro milioni 150 na kifurushi cha euro milioni 105 kwa usimamizi wa uhamiaji kwa mwaka 2023.

EU inapanga kupeleka boti, rada, kamera na magari hadi Tunisia ifikapo majira ya joto ili kuisaidia kuimarisha udhibiti wa mipaka yake ya baharini na nchi kavu. Kuongezeka kwa ushirikiano wa polisi na mahakama imepangwa kupambana na mitandao ya wasafirishaji haramu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.