Pata taarifa kuu

Tunisia: Wahamiaji waliofukuzwa Sfax watakiwa kupewa 'makazi ya dharura'

Mashirika yasiyo ya kiserikali ya Tunisia siku ya Ijumaa yalipaza sauti kutokana na hali ya "janga" linalowakabili wahamiaji kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara waliofukuzwa katika mji wa Sfax, katikati mwa nchi hiyo, yakitoa wito wa "kuwapa makaazi ya dharura" katika vituo vya mapokezi.

Mandamano ya kuwaunga mkono wahamiaji, Julai 14, 2023 huko Tunis.
Mandamano ya kuwaunga mkono wahamiaji, Julai 14, 2023 huko Tunis. © FETHI BELAID / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ijumaa jioni, waandamanaji zaidi ya mia moja waliingia katika mitaa ya Tunis kwa wito wa kundi linalopinga ufashisti kueleza "mshikamano wao na wahamiaji wasio na vibali". "Nchi ya polisi kandamizi ambayo inawafukuza na kutukandamiza", "Tunisia ni nchi ya Kiafrika, hapana kwa ubaguzi wa rangi", "Down with fascism", waliimba waandamanaji.

Kufuatia makabiliano yaliyogharimu maisha ya raia mmja wa Tunisia mnamo Julai 3, mamia ya wahamiaji wa Kiafrika walifukuzwa katika mji wa Sfax, mji wa pili kwa ukubwa nchini Tunisia na ambao mwaka huu umekuwa kitovu kikuu cha wahamiaji haramu kuondoka kwenda Ulaya.

Kisha walichukuliwa na mamlaka, kulingana na mashirika yasiyo ya kiserikali, hadi maeneo yasiyofaa karibu na nchi ya Libya upande wa mashariki na Algeria upande wa magharibi.

Bila maji, chakula au malazi, wakiwa katika joto kali ya nyuzi 40, wengi walifariki, shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Rights Watch lilisema katika taarifa hivi karibuni.

Kati ya wahamiaji 100 hadi 150, wakiwemo wanawake na watoto, bado wako katika eneo la kijeshi kwenye mpaka wa Libya, bila msaada wowote, Romdane Ben Amor, msemaji wa FTDES, shirika lisilo la kiserikali nchini Tunisia lililobobea katika masuala ya uhamiaji, amesema.

Takriban wahamiaji 165, waliotelekezwa karibu na mpaka wa Algeria, badala yake walichukuliwa na kupelekwa mahali pasipojulikana, ameongeza.

"Wahamiaji wanahamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine, na makundi mengine, wakiwa katika hali mbaya, hujificha porini kwa hofu ya kuwa na hatima sawa na wale waliokwama kwenye mipaka", amebainisha Bw. Ben Amor, akitaka wapatiwe msaada, hususan malazi ya dharura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.