Pata taarifa kuu

Idadi kubwa ya wahamiaji kutoka Tunisia wawasili Lampedusa

Takriban wahamiaji 1,800 waliokuwa kwenye boti 63 waliwasili Lampedusa mwishoni mwa juma kulingana na mamlaka ya kisiwa hicho.

Wahamiaji wapokea mahitaji ya kwanza kabla ya kupanda boti huko Lampedusa, Juni 8, 2023.
Wahamiaji wapokea mahitaji ya kwanza kabla ya kupanda boti huko Lampedusa, Juni 8, 2023. AFP - VINCENZO PINTO
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Tunis, Lilia Blaise

Hii ni idadi kubwa mno wakati idadi ya waliowasili tangu mwanzoni mwa mwaka ni karibu 110,000. Wahamiaji waliofika mwisho mwishoni mwa wiki hii wanatoka hasa Tunisia kwa mujibu wa mamlaka ya Italia, wakati nchi hiyo ilihitimisha makubaliano Julai 16 na Umoja wa Ulaya, kuimarisha mapambano yake dhidi ya wahamiaji haramu, baada ya kupewa msaada wa haraka wa euro milioni 105.

Wahamiaji wengi waliokamatwa wikendi hii waliwasili kutoka maeneo kadhaa za Tunisia: Zarzis na Djerba kusini mwa nchi, Sfax na Mahdia mashariki. Wahamiaji wasiopungua 500 waliwasili kwa siku moja. Lampedusa imejaa wahamiaji na wahamiaji wengi wamelazimika kuhamishiwa katika visiwa vya Sicily.

Takwimu za hivi karibuni zinaonyesha mipaka ya sera za Tunisia za katika suala la kudhibiti uhamiaji haramu. Kikosi cha walinzi wa taifa wa Tunisia wanasema kuwa wamekamata takriban maeneo 34,000 ya kuvukia kuelekea Bahari ya Mediterania tangu mwanzoni mwa mwaka huu, lakini hawana budi ila kuwaachilia wahamiaji hao mara tu wanapofika bandarini, kutokana na ukosefu wa miundombinu ya kuwapokea. Waziri wa Mambo ya Ndani wa Tunisia amekadiria kuwa karibu wahamiaji haramu 80,000 wako nchini Tunisia, wakiwemo 17,000 katika mji wa Sfax.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.