Pata taarifa kuu

Madagascar: Mawaziri watatu wanaohusika watimiliwa kwenye nyadhifa zao

Tangu Jumapili jioni, Madagascar imekuwa na serikali mpya inayoundwa na wizara 27. Pamoja na wahudumu wachache ambao hawajaweza kuondolewa kwa miaka mitano, sura mpya zimeonekana. Hiki ndicho kisa cha maafisa watatu wakuu ambao sasa watashughulikia nyadhifa hizo tatu zinazohusika na usalama wa nchi.

Maafisa wa polisi waMadagascar wakitawanya maandamano yaliyopigwa marufuku huko Antananarivo, mwaka wa 2019.
Maafisa wa polisi waMadagascar wakitawanya maandamano yaliyopigwa marufuku huko Antananarivo, mwaka wa 2019. AFP - RIJASOLO
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu huko Antananarivo, Sarah Tétaud

Mawaziri kumi na wawili kutoka baraza la mawaziri la zamani la mkuu wa serikali Christian Ntsay hawakupewa tena nafasi ya kuendelea kuhudumu kwenye nafasi zao. Mawaziri wanaohusika na usalama ni miongoni mwa mawaziri hao kumi na wawili ambao hawakupewa nafasi ya kuendelea kuhudumu kwenye baraza jipya la mawaziri: Waziri wa Ulinzi, Waziri wa Usalama wa Umma na vile vile waziri mwenye dhamana ya kikosi cha askari. Inavyoonekana baadhi ya mawaziri wameadhibiwa na wengine wamepongezwa kwa kubakizwa kwenye nafasi zao," kimebaini chanzo kilicho karibu na vikosi vya majeshi.

Kulingana na chanzo hiki, Waziri wa zamani wa Usalama wa Umma "amechukuliwa hatua ya kutoendelea kuhudumu kwenye nafasi yake kwa kukataa kushiriki katika ukandamizaji uliofanywa na polisi wakati wa kipindi wa uchaguzi". Nafasi yake imechukuliwa na Mdhibiti Mkuu wa Polisi Herilala Rakotoarimanana, ambaye awali alikuwa mkurugenzi wa Utafiti na mafunzo yanayoendelea ndani ya wizara.

Mkuu wa "Wizara ya Majeshi" iliyopewa jina jipya, ni mkuu wa zamani wa majeshi , Jenerali Sahivelo Delphin anayechukua nafasi hiyo. “Uteuzi mzuri,” wanasema waangalizi kadhaa walio karibu na jeshi, “kwa yule ambaye aliweza kudumisha utulivu wakati wa uchaguzi bila kuripotiwa vifo vyovyote.”

Hatimaye, idara ya kikosi cha askari "gendarmerie", ambayo hadi wakati huo ilinufaika tu na sekretarieti ya serikali, imebadilishwa a kuwa wizara. Jenerali Andry Rakotondrazaka, nambari mbili wa zamani wa idara hii, anakuwa Waziri-Mjumbe. Wengi wanamchukulia kuwa mtoto wa Jenerali Richard Ravalomanana, rais wa sasa wa Bunge la Seneti na aliye karibu na Andry Rajoelina.

Ni maafisa hawa wakuu watatu katika jeshi na polisi ndio hawa watatu waliopewa dhamana ya kudumisha utulivu na usalama nchini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.