Pata taarifa kuu

Afrika Kusini: Thabo Mbeki yuko hai: Wakfu wake

Nairobi – Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki, yuko hai na salama kwa mujibu wa wakfu wake.

Mbeki alichukua uongozi kutoka kwa rais wa kwanza kwa Afrika kusini mweusi Nelson Mandela
Mbeki alichukua uongozi kutoka kwa rais wa kwanza kwa Afrika kusini mweusi Nelson Mandela AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakfu huo umekuwa ukijibu madai yanayosambaa mitandaoni kuwa hali ya afya ya kiongozi huyo wa zamani ni mbaya, baadhi wakidai kuwa amefariki.

Hii sio mara ya kwanza kwa Mbeki kulengwa na taarifa za uongo kuhusiana na afya yake.

Mwaka wa 2021, wakati wa janga la uviko 19, taarifa za kupotosha kwenye mitandao ya kijamii zilidai kuwa rais huyo wa zamani alikuwa amefariki.

Mbeki alichukua uongozi kutoka kwa rais wa kwanza kwa Afrika kusini mweusi Nelson Mandela.

Aliongoza Afrika kusini kama rais wa pili kuchaguliwa kidemokrasia tangu mwaka wa 1999 hadi 2008.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.