Pata taarifa kuu

Viongozi wa Afrika kujaribu tena kuzungumza na Putin

NAIROBI – Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, amesema viongozi wa Afrika watatumia mkutano wa bara hilo na Urusi unaotarajiwa kufanyika Alhamisi na Ijumaa ya wiki hii, kujaribu kupata suluhu ya mzozo wa Ukraine.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa REUTERS - ESA ALEXANDER
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wake, Vincent Magwenya, amesema katika mkutano huu wa pili, viongozi watajadiliana tena na rais Vladmir Putin kuona ikiwa suluhu inaweza kupatikana ikiwemo mkataba wa usafirishaji wa nafaka ambao Moscow imejitoa.

Mkutano huu utatoa fursa kwa wakuu wa nchi za Afrika, ambao walikuwa ni sehemu ya ujumbe wa amani, kuendelea na mazungumzo na Putin kuhusu namna bora ya kupata suluhu kati ya Urusi na Ukraine.

Kikao hicho kitaangazia ushirikiano katika nyanja ya kisiasa, usalama, biashara, sayansi, teknolojia ya habari, msaada wa kibinadamu, elimu, utamaduni, michezo, vijana pamoja na mazingira.

Masuala mengine yatakayoangaziwa ni kuimarisha ushirikiano katika kupambana na ugaidi.

Afrika Kusini pia itatumia kongamano hili, ili kuweka mipango ya mwisho kabla ya kuandaliwa kwa mkutano wa BRICS mwezi ujao.

Mkutano huu unaenda kufanyika wakati huu Urusi ikijaribu kuongeza ushawishi wake barani Afrika baada ya kuwekewa vikwazo na nchi za magharibi.

Kongamano la kwanza lenye nia ya kuimarisha ushirikiano kati ya Urusi na bara la Afrika, lilifanyika Oktoba mwaka 2019, na kujitolea kuendelea kukutana kila baada ya miaka 3.

Mapema mwaka huu, rais Ramaphosa, aliongoza ujumbe wa viongozi wa Afrika katika kutafuta suluhu kuhusu mzozo kati ya Urusina Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.