Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Somalia: Kambi ya kijeshi yakumbwa na shambulio wakati vikosi vya AU vikianza kuondoa

Waislamu wenye itikadi kali wa Al-Shabab wameshambulia kambi ya kijeshi iliyoko kilomita 450 magharibi mwa mji mkuu wa Somalia Mogadishu siku ya Jumatano, polisi na mashahidi wamesema, wakati jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) likianza kuondoka nchini humo.

Katika ripoti kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Februari, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa  Antonio Guterres alisema kuwa mwaka 2022 umekuwa mwaka mbaya zaidi kwa raia nchini Somalia tangu 2017, hasa kutokana na mashambulizi ya Al-Shabab.
Katika ripoti kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Februari, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema kuwa mwaka 2022 umekuwa mwaka mbaya zaidi kwa raia nchini Somalia tangu 2017, hasa kutokana na mashambulizi ya Al-Shabab. Β© Feisal Omar / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Al-Shabab, ambao wamedai kuhusika na shambulio hilo katika taarifa kwa vyombo vya habari, walianzisha mashambulizi kadhaa ya kujitoa mhanga dhidi ya kambi ya Bardhere ambako wanajeshi wa Ethiopia na Somalia wanapatikana. "Kuna waathiriwa kadhaa, lakini hatuna maelezo ya kina hadi sasa," Abdi Bare, afisa wa polisi kutoka Bardhere, ameliambia shirika la habari la AFP, akiongeza kuwa hali "imerejea kuwa shwari". Mkazi wa Bardhere, Bare Hassan amethibitisha kutokea kwa shambulio hilo, akitaja "milio ya risasi".

Somalia, mojawapo ya nchi maskini zaidi duniani, imekuwa ikikabiliwa na mashambulizi kwa zaidi ya miaka 15 ya Waislamu wenye itikadi kali wa Al-Shabab wenye mafungamano na Al-Qaeda wanaotaka kuanzisha sheria za Kiislamu. Ili kukabiliana na uasi huu, Umoja wa Afrika ulituma mwaka 2007 kikosi kilichoundwa na askari 20,000, polisi na raia kutoka Uganda, Burundi, Djibouti, Ethiopia na Kenya, inayoitwa AMISOM.

ATMIS kisha ilichukua hatamu kutoka kwa AMISOM mnamo mwezi Aprili 2022, kwa lengo la kukabidhi jukumu kamili la usalama wa nchi kwa vikosi vya Somalia hadi mwisho wa mwaka 2024.

Shambulio hili jipya linalodaiwa na Al-Shabaab linakuja wakati ATMIS "ikianza kuondoka" nchini Somalia, kwa mujibu wa azimio la Umoja wa Mataifa linaloidhinisha kuondolewa kwa "askari 2,000 ifikapo mwisho mwa mwezi Juni 2023", kulingana na taarifa iliyotolewa Jumatano kutoka jeshi la Umoja wa Afrika.

Wanajeshi wa Somalia wamechukua hatamu kutoka kwa vikosi vya ATMIS kwenye kambi moja katika jimbo la Hirshabelle, katikati mwa nchi, taarifa hiyo imeongeza.

Rais wa Somalia Hassan Cheikh Mohamoud alitangaza "vita kamili" dhidi ya Al-Shabab, na kuanzisha mashambulizi ya kijeshi mwezi Septemba, hasa yakisaidiwa na mashambulizi ya anga ya Marekani. Lakini Al-Shabab wanaendelea kufanya mashambulizi ya umwagaji damu kwa kulipiza kisasi, wakisisitiza uwezo wao wa kushambulia katikati ya miji ya Somalia na vituo vya kijeshi.

Mwishoni mwa Mei, Al-Shabab walidai kuhusika na shambulio dhidi ya kambi iliyokuwa ikishikiliwa na wanajeshi wa Uganda kutoka Umoja wa Afrika huko Bulo Marer, kilomita 120 kusini magharibi mwa Mogadishu. Kulingana na mamlaka ya Uganda, wanajeshi 54 waliuawa katika shambulio hili, moja ya mauaji mabaya zaidi katika miezi ya hivi karibuni nchini humo.

Waislamu wenye itikadi kali pia walidai kuhusika na shambulio kwenye hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia mwezi Juni, ambalo liliua watu tisa (raia sita na maafisa watatu wa vikosi vya usalama).

Huku mashambulizi ya Al-Shabab yakizidi na kuenea hadi nchi jirani ya Kenya, Hassan Cheikh Mohamoud alimfuta kazi mkuu wa jeshi la Somalia siku ya Jumatatu.

Katika ripoti kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Februari, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Β Antonio Guterres alisema kuwa mwaka 2022 umekuwa mwaka mbaya zaidi kwa raia nchini Somalia tangu 2017, hasa kutokana na mashambulizi ya Al-Shabab.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.