Pata taarifa kuu

Somalia: Al Shabab yafanya shambulizi dhidi ya hoteli katika mji mkuu Mogadishu

Waislam wenye itikadi kali wa Al-Shabab wanafanya shambulizi linaloendelea katika hoteli moja ya mji mkuu Mogadishu siku ya Ijumaa, Juni 9, 2023, serikali na mashahidi wamesema huku, wakisema milipuko na milio ya risasi vinaendelea kusikika. 

Maafisa wa usalama wa Somalia, hapa wakishika doria Mogadishu, Februari 21, 2023.
Maafisa wa usalama wa Somalia, hapa wakishika doria Mogadishu, Februari 21, 2023. AP - Farah Abdi Warsameh
Matangazo ya kibiashara

Al Shabab inafanya shambulizi katika "hoteli oja kwenye ufuo wa Lido", sehemu inayotembewa sana viongozi mbalimali wa nchi hiyo, kulingana na taarifa ya serikali, a kuongeza: "Vikosi vya usalama vimeokoa watu wengi kutoka kwa jengo hilo na operesheni bado inaendelea" .

Al-Shabab, ambayo imedai kuhusika na shambulio hilo, ikisema imelenga sehemu inayotembelewa na viongozi wa serikali, kusini mwa Mogadishu, serikali imesema katika taarifa.

"Mgahawa ulikuwa umejaa watu"

"Vikosi vya usalama vimeokoa watu wengi kutoka kwa jengo hilo na operesheni bado inaendelea," serikali imeongeza. “Nilikuwa karibu na mkahawa wa Pearl Beach (kwenye ufuo wa Lido) wakati mlipuko mkubwa ulipotokea mbele ya jengo hilo. Nilifanikiwa kutoroka, lakini kulikuwa na milio ya risasi na askari wa usalama wakakimbilia katika eneo hilo,” shahidi wa shambulio hilo, Abdirahim Ali, ameliambia shirika la habari la AFP. “Mgahawa huo ulikuwa umejaa watu kwa sababu ulifanyiwa ukarabati hivi karibuni,” amesema Yaasin Nur, shahidi mwingine, ambaye amesema alikuwa na wasiwasi na wenzake wawili waliokuwa eneo la tukio na “hawapokei tena simu zao.

Mnamo Agosti 2020, Al shabab ilianzisha shambulio kubwa dhidi ya Elite, hoteli nyingine inayopatikana kwenye ufuo wa Lido, na kuua raia kumi na afisa mmoja wa polisi. Ilichukua vikosi vya usalama saa nne kurejesha udhibiti wa jeno hilo. Kundi la Al Shabab, lenye mafungamano na Al-Qaeda na linalodai kuanzishwa kwa sheria za Kiislamu nchini humo, limekuwa likipigania kwa zaidi ya miaka kumi na tano na serikali ya shirikisho inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa. Baada ya kutimuliwa nje ya miji mikubwa ya nchi mwaka 2011-2012, wamebaki imara katika maeneo makubwa ya vijijini.

'Vita kamili'

Rais wa Somalia Hassan Cheikh Mohamoud alitangaza "vita kamili" dhidi yao, na alianzisha mashambulizi ya kijeshi mwezi Septemba, hasa yakiungwa mkono na mashambulizi ya anga ya Marekani. Lakini Al Shabab wanaendelea kufanya mashambulizi ya umwagaji damu kwa kulipiza kisasi, wakisisitiza uwezo wao wa kushambulia katikati ya miji ya Somalia na vituo vya kijeshi. Mnamo Mei 26, walishambulia kambi iliyokuwa ikishikiliwa na wanajeshi wa Uganda kutoka Jeshi la Umoja wa Afrika nchini Somalia (Atmis) kusini mwa nchi hiyo na kuua takriban wanajeshi 54.

Mnamo Oktoba 29, 2022, mabomu mawili yaliyokuwa yametegwa katika gari yalilipuka huko Mogadishu, na kuua watu 121 na kujeruhi 333, shambulio baya zaidi kuwahi kutokea tangu miaka mitano iliyopita katika nchi hiyo ambayo pia iliyoathiriwa na ukame wa kihistoria. Mashambulio matatu huko Beledweyne (katikati) pia yaliuwa watu 30, wakiwemo maafisa wa eneo hilo, mwanzoni mwa Oktoba na takriban wageni 21 wa hoteli moja mjini Mogadishu waliuawa wakati hoteli hiyo ilipozingirwa na Al Shabab kwa saa 30 mwezi Agosti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.