Pata taarifa kuu

Somalia: Al shabaab washambulia kituo cha kijeshi cha umoja wa Afrika

NAIROBI – Nchini Somalia, wapiganaji wa kundi la kiislamu la Al shabaab, wamevamia kituo cha kijeshi cha umoja wa Afrika cha Bolu Marer, kusini magharibi mwa mji mkuu wa Mogadishu.

Wapiganaji wa Al shabaab nchini Somalia
Wapiganaji wa Al shabaab nchini Somalia AP - Farah Abdi Warsameh
Matangazo ya kibiashara

Nchini Somalia, wapiganaji wa kundi la kiislamu la Al shabaab, wamevamia kituo cha kijeshi cha umoja wa Afrika cha Bolu Marer, kusini magharibi mwa mji mkuu wa Mogadishu.

Kulingana na vikosi vya umoja huo vinavyojulikana kama ATMIS, wapiganaji hao walivamia kituo hicho kilichoko kilomita 120 kusini magharibi mwa mji mkuu wa Mogadishu.

Shambulio hilo lililenga wanajeshi wa Uganda UPDF, wanaohudumu katika kikosi hicho nchini Somalia, kwa mujibu wa msemaji wa UPDF Felix Kulayigye.

Hata hivyo, ATMIS kupitia ukurasa wake wa Twitter, haikutaja iwapo kulikuwa na waathiriwa lakini ikasema inatathmini hali kufuatia shambulio hilo.

Kwa upande wake kamanda wa jeshi la Somalia, Mohamed Yerow Hassan, wapiganaji hao wamedhibtiwa na hali ya kawaida kurejea.

Kwa zaidi ya miaka 15, wapiganaji hao wanaohusishwa na kundi la kigaidi la Al Qaeda, wamekuwa wakiendeleza mashambulio dhidi ya serikali kuu katika taifa hilo la pembe ya Afrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.