Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Somalia: Watu 22 wafariki katika ulipuaji wa mabomu ambayo hayakulipuka

Watu 22, wakiwemo watoto wawili, wameuawa katika mlipuko wa mabomu ambayo hayakulipuka nchini Somalia, yapata kilomita 120 kusini mwa mji mkuu Mogadishu, naibu mkuu wa wilaya amesema siku ya Ijumaa. "Kumetokea maafa karibu na Qoryoley, watoto wasio na hatia wameuawa katika mlipuko uliosababishwa na mabomu," ameongeza afisa wa serikali, Abdi Ahmed Ali, wakati wa mkutano na waandishi wa habari akionukuliwa na shirika la habari la AFP.

Al Shabab ambao walifukuzwa nje ya miji mikubwa mwaka 2011-2012, wamesalia imara katika maeneo makubwa ya vijijini, ambapo wanaendelea kufanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama na ulinzi bila kusahau kiraia.
Al Shabab ambao walifukuzwa nje ya miji mikubwa mwaka 2011-2012, wamesalia imara katika maeneo makubwa ya vijijini, ambapo wanaendelea kufanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama na ulinzi bila kusahau kiraia. ABDIHALIM BASHIR via REUTERS - ABDIHALIM BASHIR
Matangazo ya kibiashara

Naibu kamishna hakubainisha ni wapi vifaa hivi vya kijeshi vilitoka, au wakati viliwekwa au kutua kwenye eneo hilo.

Risasi na mabomu 'vilitawanywa katika mkoa'

Eneo hilo ni eneo la mapigano ya mara kwa mara kati ya vikosi vya Somalia, vinavyoungwa mkono na kikosi cha Umoja wa Afrika (AU), na Waislam wenye itikadi kali wa Al-Shabab wenye mafungamano na Al-Qaeda, ambao wamekuwa wakipigana na serikali ya shirikisho inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa tangu mwaka 2007. Abdi 

Ahmed Ali aliomba mamlaka msaada "kuondoa mabomu haya ambayo hayakulipuka ambayo yametawanyika katika mkoa mzima" na "kuepusha majanga haya". Mkazi wa jiji hilo, Ibrahim Hassan, aliyehojiwa na shirika la habari la AFP, amesema kuwa wengi wa waathiriwa walikuwa "watoto wadogo, ambao walikufa papo hapo baada ya mmoja wao kukanyaga kilipuzi karibu na uwanja wa michezo".

Mnamo Mei 26, wanajeshi wasiopungua 54 waliuawa na wapiganaji wa Al Shabab ambao walishambulia kambi ya Umoja wa Afrika (AU) iliyokuwa ikishikiliwa na wanajeshi wa Uganda huko Bulo Marer, mji ulio umbali wa kilomita 30 kutoka Qoryoley. Al Sabab imekuwa ikipigana kwa zaidi ya miaka kumi na tano na serikali ya Somalia inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa, ili kuanzisha sheria ya Kiislamu katika nchi hii ya Pembe ya Afrika. Al Shabab ambao walifukuzwa nje ya miji mikubwa mwaka 2011-2012, wamesalia imara katika maeneo makubwa ya vijijini, ambapo wanaendelea kufanya mashambulizi dhidi ya vikosi vya usalama na ulinzi bila kusahau kiraia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.