Pata taarifa kuu

Somalia: Al-Shabab yadai kufanya shambulio dhidi ya kambi ya jeshi la Umoja wa Afrika

Wanamgambo wa Kiislam wenye itikadi kali wa Al-Shabab wamedai kuhusika na shambulio lililotekelezwa Ijumaa hii, Mei 26, dhidi ya kambi ya wanajeshi wa Uganda wa kikosi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (Atmis), Atmis na msemaji wa jeshi la Uganda wametangaza, bila maelezo zaidi au kutoa idadi ya wanajeshi waliouawa au kujeruhiwa.

Mji wa Bulo Marer, Somalia.
Mji wa Bulo Marer, Somalia. © FMM
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu jijini Nairobi, Florence Morice

Kambi ya Jeshi la Atmis, iliyoko Bulo Marer, kilomita 120 kusini mwa Mogadishu kando ya pwani, ambako kunapatikana kikosi cha jeshi la Uganda, ndio iliyoshambuliwa. Shambulio hilo lilifanyika "mapema asubuhi", kulingana na msemaji wa jeshi la Uganda. Karibu saa 11 asubuhi, anasema kamanda wa Atmis, kikosi cha Umoja wa Afrika kwa Somalia.

Awali, mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua kwenye gari lililokuwa na 'vilipuzi' kabla ya mapigano kuanza kwa "silaha za kiotomatiki", kamanda wa jeshi ameliambia shirika la habari la AFP. Vyombo vya habari vya ndani pia vinaripoti kuwa milipuko ilisikika muda mfupi baada ya shambulio hilo kuanza.

Shambulio kubwa la mwisho dhidi ya Atmis lilitokea Mei 2022, mwaka mmoja uliopita. Shebab walishambulia kambi iliyokuwa ikishikiliwa na wanajeshi wa Burundi. Umoja wa Afrika ulikuwa haujatoa taarifa zozote za kulipiza kisasi lakini vyanzo vya jeshi la Burundi vilitoa idadi ya wanajeshi 45 waliouawa au kutoweka. Mashambulizi dhidi ya kambi za kikosi hiki yanafasiriwa mara kwa mara kama ujumbe unaokusudiwa kuharakisha kuondoka kwa kikosi hicho kutoka Somalia. Jukumu la sasa la Atmis linatoa ukomo wake ifikapo mwisho wa mwaka 2024.

Mashambulizi yaliyoanzishwa majira ya joto yaliyopita na rais mpya yameiwezesha Mogadishu kuteka tena maeneo makubwa katikati mwa nchi hiyo katika majimbo ya Hirshabelle na Galmudug. Tangu wakati huo, Al Shebab wameendelea kufanya mashambulizi mabaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.