Pata taarifa kuu

Kimbunga Freddy: Malawi yatangaza wiki mbili za maombolezo ya kitaifa

Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera, ametangaza Jumatano hii, Machi 15, 2023 wiki mbili za maombolezo ya kitaifa baada ya watu zaidi ya 200 kuuawa na Kimbunga Freddy katika nchi hii maskini ya kusini mwa Afrika.

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera
Rais wa Malawi Lazarus Chakwera AMOS GUMULIRA / AFP
Matangazo ya kibiashara

 

“Kutokana na ukubwa wa vifo vilivyosababishwa na maafa haya, nimeamua sisi sote kama taifa kufanya siku 14 za maombolezo na bendera zote zipeperushwe nusu mlingoti kwa siku saba za mwanzo,” amesema Lazaro Chakwera katika hotuba yake kwa taifa.

Baada ya kupiga kwa mara ya pili mwishoni mwa juma nchini Msumbiji, na kuua takriban watu 10, mapema siku ya Jumatatu Kimbunga Freddy kilielekea kusini mwa Malawi. Hali ya maafa imetangazwa katika eneo la Blantyre, mji mkuu wa kiuchumi kitovu cha janga hili.

Nchi ambayo hadi sasa imepata hasara kubwa baada ya kurejea kwa kimbunga cha kitropiki, ambacho kimefuata mkondo wa kitanzi ambao haujaorodheshwa na wataalamu wa hali ya hewa, sasa kimeua 'watu 190 na wengine 584 wamejeruhiwa na 37 hawajulikani waliko,' Ofisi ya Taifa inayohusika na Kukabiliana na Majanga imetangaza katika taarifa.

Ripoti ya awali iliripoti vifo vya watu 99 na inaweza kuongezeka zaidi kadri utafiti unavyoendelea. Katika kitongoji cha Chilobwe, karibu na Blantyre, wakazi waliopigwa na butwaa walisimama mbele ya mabaki ya nyumba zilizosombwa na maporomoko ya udongo. Upepo ulipungua lakini mvua inaendelea kunyesha.

Takriban watu 20,000 nchini humo wameathiriwa na hali mbaya ya hewa, kulingana na Umoja wa Mataifa. Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alisema katika taarifa yake "amesikitishwa na watu kupoteza maisha". Kimbunga Freddy kilipiga bara la Afrika kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi Februari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.