Pata taarifa kuu

Idadi ya waliofariki kutokana na kimbunga Freddy yaongezeka hadi 190 nchini Malawi

Kimbunga Freddy, chenye rekodi ya maisha marefu na ambacho kimepiga mara mbili kusini mwa Afrika, kinaendelea kusababisha maafa nchini Malawi, huku ripoti ya hivi punde Jumanne ikiripoti vifo vya angalau watu 190 katika nchi hii maskini na isiyo na bahari.

Wakazi wakitazama uharibifu uliosababishwa na Kimbunga Freddy huko Chilobwe, Blantyre, Malawi mnamo Machi 13, 2023.
Wakazi wakitazama uharibifu uliosababishwa na Kimbunga Freddy huko Chilobwe, Blantyre, Malawi mnamo Machi 13, 2023. REUTERS - ELDSON CHAGARA
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kupiga kwa mara ya pili mwishoni mwa juma nchini Msumbiji, na kuua takriban watu 10, mapema siku ya Jumatatu Kimbunga Freddy kilielekea kusini mwa Malawi. Hali ya maafa imetangazwa katika eneo la Blantyre, mji mkuu wa kiuchumi kitovu cha janga hili.

Nchi ambayo hadi sasa imepata hasara kubwa baada ya kurejea kwa kimbunga cha kitropiki, ambacho kimefuata mkondo wa kitanzi ambao haujaorodheshwa na wataalamu wa hali ya hewa, sasa kimeua 'watu 190 na wengine 584 wamejeruhiwa na 37 hawajulikani waliko,' Ofisi ya Taifa inayohusika na Kukabiliana na Majanga imetangaza katika taarifa.

Ripoti ya awali siku moja kabla iliripoti vifo vya watu 99 na inaweza kuongezeka zaidi kadri utafiti unavyoendelea. Katika kitongoji cha Chilobwe, karibu na Blantyre, wakazi waliopigwa na butwaa walisimama mbele ya mabaki ya nyumba zilizosombwa na maporomoko ya udongo. Upepo ulipungua lakini mvua inaendelea kunyesha.

"Hatuna msaada na hakuna mtu wa kutusaidia," John Witman, 80, ameliambia shirika la habari la AFP. Anamtafuta mkwewe, ambaye alitoweka baada ya nyumba yake ikupoporomoka, na kusombwa na maji yaliyokuwa yakipanda ghafla.

Wakaazi wanasema wanaamini makumi ya miili ingali humo, iliyozikwa kwenye matope. Wachimbaji wametumwa katika baadhi ya maeneo. Siku moja kabla, familia na waokoaji walitafuta miili ya watu chini ya matope, huku wakifukuwa udongo kwa mikono mitupu katika mvua iliyokuwa ikinyesha.

Idadi kubwa ya watu wapelekwa Hospitali

Hospitali katika mkoa huo "imezidiwa na wimbi la majeruhi", shirika la Madaktari Wasio na Mipaka, limeonya katika taarifa. "Hospitali kuu ya Malkia Elizabeth pekee imepokea watu 220, wakiwemo watu wazima 42 na watoto 43 ambao walitangazwa kufariki walipofika." Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka linahofia hasa kuzuka tena kwa kipindupindu.

Takriban watu 20,000 nchini humo wameathiriwa na hali mbaya ya hewa, kulingana na Umoja wa Mataifa. Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alisema katika taarifa yake "amesikitishwa na watu kupoteza maisha". Kimbunga Freddy kilipiga bara la Afrika kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi Februari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.