Pata taarifa kuu

Mkataba wa ziada kati ya Rwanda na Msumbiji wawatia wasiwasi watu wanaoishi nje ya nchi

Wakimbizi wa Rwanda na wanaotafuta hifadhi nchini Msumbiji wamrelezea wasiwasi wao siku ya Jumatano kabla ya kuidhinishwa kwa mkataba wa kuwarejesha nyumbani watu wanaoshtumiwa kufanya makosa kati ya nchi hizo mbili za Afrika, wakihofia kuwa unaweza kutumika kuwatesa wapinzani walio uhamishoni.

Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Rais wa Rwanda Paul Kagame. REUTERS - JEAN BIZIMANA
Matangazo ya kibiashara

 

Nakala hiyo, iliyotiwa saini mjini Kigali mwezi Juni mwaka jana, iliidhinishwa rasmi na serikali ya Msumbiji siku ya Jumanne, na kuandaa njia ya kuidhinishwa na Baraza la Wawakilishi. Bunge la Seneti la Rwanda kwa upande wake liliidhinisha mkataba huo mapema wiki hii.

Rwanda inashutumiwa mara kwa mara kwa kuwawinda wapinzani walio uhamishoni, tuhuma ambayo imekuwa ikikanusha kila mara. "Makubaliano haya yanatisha," msemaji wa Chama cha Wakimbizi wa Rwanda nchini Msumbiji ameliambia shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina.

"Tungependa itumike kwa madhumuni ya haki, lakini matukio ya hivi karibuni yanatufanya tuamini kwamba inahusu zaidi mateso," ameongeza. Wapinzani kadhaa wa Rwanda wameuawa au kutoweka baada ya kutekwa nyara kusini mwa Afrika katika miaka ya hivi karibuni.

Hasa nchini Msumbiji: Luteni wa zamani wa Rwanda alipigwa risasi na kufa katika kitongoji cha Maputo mwaka 2021, na mwaka 2012 mwili wa mkuu wa zamani wa Benki ya Maendeleo ya Rwanda ulipatikana ukielea baharini karibu na mji mkuu. Msemaji wa serikali ya Msumbiji Filimao Suazi amesema mkataba huo wa kuwarejesha watu nchini humo unahusu uhalifu na hukumu zilizopita na zijazo.

Maelfu ya wakimbizi wa Rwanda wanaishi Msumbiji, kulingana na Umoja wa Mataifa. Wengi wao waliishi nchini humo baada ya mauaji ya halaiki ya Rwanda mwaka 1994 ambayo yaligharimu maisha ya watu wapatao 800,000. Tangu wakati huo, Rais wa Rwanda Paul Kagame ameitawala nchi yake kwa mkono wa chuma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.