Pata taarifa kuu

Mafuta: Libya yakaribisha makampuni ya kigeni kuanza tena shughuli zao

Kampuni ya taifa ya mafuta nchini Libya (NOC) imetoa wito kwa makampuni ya kigeni yanayofanya kazi katika sekta ya hidrokaboni kuanza tena shughuli zao za uchunguzi na uzalishaji, ikitaja kuboreshwa kwa hali ya usalama.

Wanajeshi wakidumisha usalama katika makao makuu ya Kampuni ya taifa ya Mafuta nchini Libya (NOC), mjini Tripoli mnamo Julai 14, 2022.
Wanajeshi wakidumisha usalama katika makao makuu ya Kampuni ya taifa ya Mafuta nchini Libya (NOC), mjini Tripoli mnamo Julai 14, 2022. © Hazem Ahmed / Reuters
Matangazo ya kibiashara

"NOC inatoa wito kwa makampuni ya kimataifa yanayofanya kazi katika sekta ya mafuta na gesi, ambayo makubaliano ya uchunguzi na uzalishaji wa mafuta na gesi yametiwa saini, kuondoa nguvu iliyotumiwa kwa upande wao," kulingana na taarifa iliyotolewa usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne.

"Hali ya dharura" ni hatua inayotumika katika hali za kipekee, kuruhusu kusamehewa dhima ya NOC, au katika kesi hii, makampuni yanayofanya kazi nchini Libya, katika tukio la kutofuata majukumu ya kimkataba.

Katika muongo mmoja uliopita, Libya imekuwa ikikumbwa mara kwa mara na mapigano makali kati ya pande hasimu kutoka Mashariki na Magharibi, ambayo yameathiri uchimbaji wa mafuta, usafirishaji wa hidrokaboni na vituo vya mafuta, kuingizwa katika mvutano kati ya kambi hizo mbili.

NOC imebaini kwamba imetoa wito huu baada ya kufanya "tathmini" ya hali ya usalama na ikabainisha "maboresho makubwa" kwenye baadhi ya maeneo ambapo ilikuwa vigumu kufanya kazi.

NOC ilizitaka kampuni za kigeni "kuanzisha tena shughuli zao" za uchunguzi na uchimbaji, na kuwahakikishia kuwa itawapa "msaada wote muhimu" ili waweze kufanya kazi "katika mazingira salama", kwa ushirikiano na mamlaka ya kiraia na kijeshi. " 

Takriban miaka kumi na moja baada ya kuangushwa kwa Muammar Gaddafi, Libya, ambayo ina hifadhi nyingi zaidi barani Afrika, imesalia kuwa kati ya makundi hasimu kutoka mashariki na magharibi, kutokana na kuingiliwa na mataifa ya kigeni.

Tangu mwezi Machi, serikali mbili zimekuwa zikigombea madaraka, moja ikiwa na makao yake mjini Tripoli (magharibi) na kutambuliwa na Umoja wa Mataifa, nyingine ikiungwa mkono na Bunge na kambi ya Marshal Khalifa Haftar, kiongozi mwenye ushawishi mkubwa huko Mashariki.

Siku moja baada ya kuteuliwa katikati ya mwezi wa Julai kama mkuu wa NOC, Farhat Bengdara alitangaza kuondolewa kwa kizuizi kwenye maeneo sita makuu ya mafuta na vituo, vilivyofungwa na makundi yenye ushirikiano wa karibu na kambi ya mashariki tangu katikati ya mwezi wa Aprili.

Mwanzoni mwa mwezi wa Novemba, alibaini kuwa nchi yake ilikuwa inataka kuongeza uzalishaji wake wa mafuta "hadi mapipa milioni 2" kwa siku, karibu mara mbili ikilinganishwa na kiwango cha sasa cha mapipa 1.2 milioni kwa siku.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.