Pata taarifa kuu

Uhalifu uliofanywa nchini Libya: Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC azuru miji mingi

Mwanasheria Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Karim Khan, amekuwa akizuru Libya tangu Jumamosi ya wiki iliyopita. Alianza kwa kwenda katika mji wa Tarhouna, ambapo makaburi ya umati yenye miili zaidi ya 300 yaligunduliwa katika majira ya joto ya 2020. Ziara hii ni sehemu ya uchunguzi wa uhalifu uliofanywa nchini Libya, kulingana na ICC, na mwendesha mashtaka alikutana na familia za waathiriwa huko Tarhuna.

Karim Khan, Julai 27,  2019.
Karim Khan, Julai 27, 2019. AFP - SABAH ARAR
Matangazo ya kibiashara

Hii ni ziara ya kwanza kwa mwendesha mashtaka mkuu wa ICC nchini Libya katika kipindi cha miaka kumi. Karim Khan alizungumza na viongozi kadhaa wa kisiasa, akiwemo Waziri wa Sheria na mwanasheria mkuu wa kijeshi mjini Tripoli. Siku ya Jumanne, alikwenda Benghazi, alikutana na Marshal Haftar, lakini hakuna kilifahamika kuhusu mkutano huo.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC ataripoti Jumatano hii, Novemba 09, kutoka Tripoli, kuhusu hali ya Libya kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Mwanasheria wa zamani wa Seif al-Islam

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu imekuwa ikichunguza uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita uliofanywa nchini Libya kwa miaka kadhaa, pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa dhidi ya wahamiaji.

Kabla ya kuwa mkuu wa taasisi hii ya kimataifa, Karim Khan alikuwa mwanasheria wa Seifal-Islam Gaddafi wakati alipokuwa akishitakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu na ICC. Mtoto wa kiume wa Gaddafi, aliyehukumiwa na kisha kupewa msamaha nchini Libya, bado hajakabidhiwa kwa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu.

Ziara hii, hata hivyo, inazua wasiwasi kwa baadhi ya raia nchini Libya. Wanahofia kwamba ziara yake nchini Libya itachukuwa sura ya kisiasa, hasa ikiwa maamuzi yanayochukuliwa huenda yakazuia baadhi ya watu kushiriki katika chaguzi zijazo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.