Pata taarifa kuu

Abdoulaye Bathily kutoka Senegal ateuliwa kuwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya

Baada ya miezi kadhaa ya wadhifa huo kuwa wazi, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amemteua mwanadiplomasia wa Senegal Abdoulaye Bathily kuwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, ambako serikali mbili zinapigania mamlaka, ofisi yake ilisema siku ya Ijumaa.

Abdoulaye Bathily ateuliwa kuwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya.
Abdoulaye Bathily ateuliwa kuwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Libya. AFP / Marco Longari
Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo wa zamani wa Senegal aliwahi kuwa mwakilishi wa Umoja wa Mataifa katika kanda ya Afrika ya Kati, mshauri maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Madagascar na naibu mwakilishi maalum wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Mali.

Mtangulizi wake, Mslovakia Jan Kubis, alijiuzulu ghafla mwezi Novemba mwaka jana. Tangu wakati huo, nafasi hiyo imekuwa wazi, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo idhini yake ni muhimu, baada ya kukataa mapendekezo kadhaa ya Katibu Mkuu.

Siku chache zilizopita, vyanzo vya kidiplomasia vililiambia shirika la habari la AFP kwamba wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa sasa walikubaliana juu ya jina la Abdoulaye Bathily. Serikali ya Tripoli, kwa upande mwingine, ilikuwa imeonyesha 'kutoridhishwa' na uteuzi huo.

Uteuzi wa mjumbe mpya ulitarajiwa hasa kwani Umoja wa Mataifa uko mstari wa mbele kuandaa upatanishi kati ya pande hizo mbili ili kufikia muafaka wa kikatiba unaoruhusu kufanyika kwa uchaguzi na  kwamba ghasia mpya ziliutikisa Tripoli mwishoni mwa mwezi wa Julai.

Serikali mbili zinawania madaraka katika nchi hiyo ya mafuta iliyotumbukia katika machafuko tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011: moja iko Tripoli (magharibi) na inaongozwa na Abdelhamid Dbeibah tangu mwanzoni mwa 2021, na nyingine ikiongozwa tangu mwezi Machi na Fathi Bachagha na kuungwa mkono na kambi ya Marshal Khalifa Haftar, mbabe wa kivita huko Mashariki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.