Pata taarifa kuu
USALAMA-SIASA

Watano wauawa katika mapigano kati ya makundi yenye silaha nchini Libya

Mapigano kati ya makundi yenye silaha yamezuka usiku kucha kuanzia Jumapili hadi Jumatatu huko Zaouia, mji ulioko magharibi mwa Libya, na kuua watu 5 na kujeruhi 13, kulingana na idara ya huduma za dharura.

Serikali mbili zimekuwa zikigombea madaraka tangu mwezi Machi: moja ikiwa na makao yake mjini Tripoli na kuongozwa na Abdelhamid Dbeibah na nyingine ikiongozwa na Fathi Bachagha na kuungwa mkono na kambi ya Marshal Khalifa Haftar, mbabe wa kivita huko Mashariki mwa nchi.
Serikali mbili zimekuwa zikigombea madaraka tangu mwezi Machi: moja ikiwa na makao yake mjini Tripoli na kuongozwa na Abdelhamid Dbeibah na nyingine ikiongozwa na Fathi Bachagha na kuungwa mkono na kambi ya Marshal Khalifa Haftar, mbabe wa kivita huko Mashariki mwa nchi. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Libya, mapigano hayo, hasa ya silaha nzito, ni kati ya makundi mawili yenye uhusiano rasmi na Wizara ya Ulinzi na Mambo ya Ndani, katikati mwa jiji hili lililoko takriban kilomita arobaini kutoka mji mkuu Tripoli.

Idara ya huduma za dharura na uokoaji imeripoti kuwa watu 5 wameuawa, akiwemo msichana wa miaka 10, na 13 kujeruhiwa.

Kwa mujibu wa chanzo cha usalama cha eneo hilo ambacho kimeomba jina lake lisitajwe, mapigano hayo yalizuka baada ya mwanachama mmoja wa makundi hayo mawili kuuawa na mfuasi wa kundi jingine kutokana na mzozo kuhusu ulanguzi wa mafuta, ambao umeenea sana katika eneo hili karibu na mpaka na Tunisia.

Mapigano haya yanatokea wakati nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika inapitia mzozo mkubwa wa kisiasa dhidi ya hali ya ukosefu wa usalama wa kudumu unaosababishwa na mapigano ya mara kwa mara kati ya makundi yenye silaha.

Serikali mbili zimekuwa zikigombea madaraka tangu mwezi Machi: moja ikiwa na makao yake mjini Tripoli na kuongozwa na Abdelhamid Dbeibah na nyingine ikiongozwa na Fathi Bachagha na kuungwa mkono na kambi ya Marshal Khalifa Haftar, mbabe wa kivita huko Mashariki mwa nchi.

Mwishoni mwa mwezi Agosti, mapigano kati ya wanamgambo hasimu huko Tripoli yalisababisha vifo vya watu 32 na 159 kujeruhiwa kutokana na mzozo huu wa kisiasa.

Libya imetumbukia katika machafuko tangu kuanguka kwa utawala wa Muammar Gaddafi mwaka 2011, uliokumbwa na vita vya kuwania madaraka na migawanyiko ya kikanda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.