Pata taarifa kuu
LIBYA

Umoja wa Mataifa wataka jitihada zifanyike kufanikisha mazungumzo ya kisiasa

Umoja wa Mataifa unataka hatua za makusudi kuchukuliwa, kati ya makundi pinzani nchini Libya, ili kupata suluhu ya kuandaa uchaguzi ambao umesubiriwa nchini humo kwa muda mrefu.

Waziri wa Mkuu wa Libya  Fathi Bachagha,
Waziri wa Mkuu wa Libya Fathi Bachagha, © Yousef Murad / AP
Matangazo ya kibiashara

Spika wa bunge  Aguila Saleh na rais wa bazara la taifa Khaled Al-Mishri wanakutana katika afisi za umoja wa mataifa, kwa siku mbili kujadili rasimu ya uchaguzi na katiba. 

Mjumbe wa Umoja wa mataifa nchini Libya, Stephanie Williams, amesema uwepo wa viongozi hao wawili kule Geneva, ni ishara wakati umewadia wa maamuzi kuchukuliwa kwa niaba ya raia wa Libya, na kuhakikisha kwamba wanaafikiana na kuandaa uchaguzi hivi karibuni. 

Mkutano wa juma moja kati ya serikali ya Tripoli na ile ya mashariki ulimaliziika juma lilipoita bila mwafaka. 

Uchaguzi wa Urais na wabunge, uliokuwa ufanyike disemba mwaka uliopita haukufanyika, na ulitarajiwa kumaliza mzozo kati ya pande hasimu nchini Libya. 

Fathi Bashagha waziri mkuu anayeungwa mkono na bunge la msahariki, jumatano iliopita alimwandikia barua katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres, kwamba atakuwa anaongoza mazungumzo ya kuhakikisha uchaguzi unafanyika nchini Libya. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.