Pata taarifa kuu

Mjumbe maalum wa UN nchini Libya ataka kuunganisha serikali kuu kabla ya uchaguzi

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Libya, Abdoulaye Bathily, raia wa Senegal, aliwasilisha kwa Umoja wa Mataifa, Jumanne, Oktoba 25, ripoti yake ya kwanza kuhusu hali katika nchi hii iliyokumbwa na machafuko kwa zaidi ya miaka kumi na moja. Aliwasili Libya, karibu wiki mbili zilizopita, amefanya mikutano mara kadhaa na maafisa mjini Tripoli.

Abdoulaye Bathily mjini Dakar, mnamo mwaka 2008.
Abdoulaye Bathily mjini Dakar, mnamo mwaka 2008. © Wikimedia Commons CC BY SA Serigne Diagne
Matangazo ya kibiashara

Mbele ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Abdoulaye Bathily alizungumzia kuhusu matokeo ya mashauriano yake na wadau mbalimali katika mzozo nchini Libya. Alipinga kufanyika kwa uchaguzi katika siku za usoni. Papo hapo, aliweza kupima "tofauti kubwa kati ya Walibya", hasa kuhusiana na msingi wa kisheria ambao utawezesha kufanyika kwa uchaguzi mkuu.

Barabara ya kuelekea uchaguzi lazima sasa ipitie muunganisho wa uongozi wa serikali na hili ndilo jukumu ambalo anatakiwa kulishughulikia kwa haraka. Serikali mbili zimekuwa zikigombea madaraka tangu mwezi Machi nchini Libya. Mjumbe huyo maalum wa Umoja wa Mataifa anapanga kuandaa mkutano kati ya spika wa bunge na mkuu wa baraza kuu la ushauri, ili kuhimiza matumizi ya makubaliano ya kuunganishwa tena kwa taasisi hizo mbili.

Kuzindua upya mijadala ya usalama

Mjumbe huyo mpya pia anataka kuzindua upya kipengele cha usalama cha mkataba wa kisiasa uliositishwa kutokana na mzozo wa madaraka. Mkutano wa kamati ya pamoja ya kijeshi ya 5+5, inayoundwa na wawakilishi watano kutoka mashariki na wengine watano kutoka magharibi mwa nchi, utafanyika yeye akihudhuria, siku ya Alhamisi tarehe 27 Oktoba huko Sirte. Lengo ni kupunguza mvutano.

Kabla ya kuondoka New York, Abdoulaye Bathily alitoa hoja ya kukutana na wawakilishi wote wa nchi zinazohusika na Libya. Kwa kufanya hivyo, alisisitiza haja na umuhimu wa kuratibiwa kwa uungaji mkono wa kimataifa kwa juhudi za Libya na Umoja wa Mataifa. Alitoa wito kwa nchi hizo kujiepusha kuchukua maamuzi ya upande mmoja ambayo yanaweza kuzidisha migawanyiko nchini Libya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.