Pata taarifa kuu

Mwendesha mashtaka wa ICC azuru Libya

Mwanasheria Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) Karim Khan yuko ziarani nchini Libya ambako ametembelea maeneo ya makaburi ya halaiki ambapo maiti kadhaa zimegunduliwa tangu majira ya joto ya 2020.

Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Karim Khan.
Mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, Karim Khan. AFP - DANIEL MUNOZ
Matangazo ya kibiashara

Wakati wa ziara yake huko Tarhouna (magharibi) siku ya Jumatatu, "katika muktadha wa uchunguzi wa uhalifu uliofanywa nchini Libya", Bw. Khan alikutana na jamaa za waathiriwa ambao mbele yao alisisitiza "dhamira yake ya kuharakisha kazi ya faili ya Libya, " ICC iliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter siku ya Jumanne.

Alipowasili Tripoli siku ya Jumamosi kwa ziara ya kwanza ya mwendesha mashtaka wa ICC katika muongo mmoja, Khan alifanya mazungumzo na maafisa kadhaa wa Libya, akiwemo Rais wa Baraza la utawala Mohamed el-Manfi, Waziri wa Sheria Halima Ibrahim na mwanasheria mkuu wa kijeshi.

Bw Khan anatarajiwa kutoa taarifa kwa njia ya video kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano kuhusu hali ya Libya, kulingana na ICC.

Hadi sasa, zaidi ya miili 270 imegunduliwa katika makaburi ya halaiki huko Tarhouna na timu kutoka Idara ya Upelelezi wa Jinai na Mamlaka Kuu ya Utafutaji na Utambuzi wa Waliopotea.

Makaburi ya kwanza ya umati yaligunduliwa baada ya kuondoka katika jiji hilomwezi Juni 2020 kwa vikosi vya Marshal Khalifa Haftar, mbabe wa kivita kutoka mashariki mwa Libya, ambaye alijaribu, bila mafanikio, tangu Aprili 2019 hadi Juni 2020, kuuteka mji mkuu Tripoli, ambapo ndio makao makuu ya serikali inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa.

Mahakama ya ICC ina historia ndefu ya kuchunguza uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita uliofanywa nchini Libya pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu unaokumba wahamiaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.