Pata taarifa kuu

Watano wauawa katika shambulizi katika kambi ya mafunzo ya kijeshi nchini Somalia

Watu watano wameuawa katika shambulio la kujitoa muhanga la wanajihadi kwenye kambi ya mafunzo ya kijeshi nchini Somalia, maafisa wa jeshi wameliambia shirika la habari la AFP leo Jumapili. Miongoni mwa wahanga pia ni raia ambao walikuwa wanakaa karibu na kambi hiyo, kulingana na afisa wa jeshi. 

Mwishoni mwa wiki iliyopita, wanamgambo walifanya mashambulizi mawili ya mabomu yaliyotegwa ndani ya gari yakilenga Wizara ya Elimu, shambulio baya zaidi kuwahi kutokea nchini humo katika kipindi cha miaka mitano.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, wanamgambo walifanya mashambulizi mawili ya mabomu yaliyotegwa ndani ya gari yakilenga Wizara ya Elimu, shambulio baya zaidi kuwahi kutokea nchini humo katika kipindi cha miaka mitano. ABDIHALIM BASHIR via REUTERS - ABDIHALIM BASHIR
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hili, lililotekelezwa siku ya Jumamosi katika kambi hii iliyoko Mogadishu, mji mkuu wa Somalia, lilidaiwa na wanajihadi wa Al-Shabaab wiki moja baada ya mashambulizi mawili yaliyosababisha vifo vya watu 116.

Haya yanajiri huku serikali ikizidisha mapambano yake dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu ambao wamekuwa wakiendesha uasi kwa miaka 15 katika nchi hii yenye machafuko iliyoko katika Pembe ya Afrika.

"Shambulio la bomu la kujitoa muhanga lilitokea kwenye lango (la kambi) na askari wapya watano walikufa katika mlipuko huo na wengine zaidi ya kumi walijeruhiwa," Mohammad Abdullahi, afisa wa jeshi ameliambia shirika la habari la AFP.

Hakuna tamko rasmi ambalo limetoka kwa serikali kuhusu shambulio lililodaiwa na Al-Shabab, ambao wapiganaji wao wenye mafungamano na al-Qaeda wameongeza mashambulizi nchini Somalia tangu Rais Hassan Sheikh Mohamud alipoingia madarakani mwezi Mei na kuapa kuanzisha "vita kamili" dhidi ya wanajihadi.

Siku ya Ijumaa, wizara ya habari ilisema jeshi limewaua zaidi ya wapiganaji 100 wa Al-Shabab katika operesheni katikati mwa jimbo la Hirshabelle.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, wanamgambo walifanya mashambulizi mawili ya mabomu yaliyotegwa ndani ya gari yakilenga Wizara ya Elimu, shambulio baya zaidi kuwahi kutokea nchini humo katika kipindi cha miaka mitano.

Shambulio hilo lilitokea katika makutano ya barabara ambapo lori lililokuwa na vilipuzi lililipuka Oktoba 14, 2017 na kusababisha vifo vya watu 512 na wengine zaidi ya 290 kujeruhiwa.

Mwezi Agosti, kundi hilo lilivamia hoteli maarufu ya Hayat mjini Mogadishu kwa takriban saa 30, na kuua watu 21 na wengine 117 kujeruhiwa.

Waasi hao ambao walitaka kupindua serikali dhaifu, walifukuzwa nje ya mji mkuu mwaka 2011 na kikosi cha Umoja wa Afrika.

Lakini kundi hilo bado linadhibiti maeneo mengi ya nchi na linaendelea kufanya mashambulizi mabaya dhidi ya malengo ya kiraia, kisiasa na kijeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.