Pata taarifa kuu

100 wafariki katika shambulio la bomu Somalia

Idadi ya watu waliokufa kutokana na mashambulio mawili ya mabomu ya kujitoa muhanga kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, imefikia watu 100, amesema rais wa nchi hiyo, Hassan Sheikh Mohamud.

Moshi ukiwa umetanda mjini Mogadishu baada ya shambulio la bomu. 29 10 2022
Moshi ukiwa umetanda mjini Mogadishu baada ya shambulio la bomu. 29 10 2022 REUTERS - FEISAL OMAR
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake, rais Mohamud, amesema hadi kufikia sasa watu waliokufa wamefikia 100 na zaidi ya 300 wamejeruhiwa, na kwamba idadi ya waliokufa na kujeruhiwa inaendelea kuongezeka.

Polisi mjini Mogadishu imesema magari mawili yaliyokuwa na vilipuzi, yalilipuka jirani na eneo maarufu la njiapanda la Zobe, baada ya kutokea makabiliano jirani na ofisi za wizara ya elimu.

Taarifa ya polisi imeongeza kuwa, mlipuko huo ulisababisha madhara makubwa kwa majengo yaliyojirani na wizara ya elimu, huku yakisababisha vumbi na moshi mkubwa angani.

Miongoni mwa waliouawa wamo wanawake, watoto na wazee, alisema msemaji wa polisi, Sadik Dudishe.

"Wanamgambo wasio na huruma wameua mama zetu, wengine na hasa watoto wakipoteza maisha kutokana na kufukiwa na vifusi", ilisema taarifa ya polisi.

Shambulio hili limetekelezwa katika eneo ambalo October 14 mwaka 2017, watu zaidi ya 500 waliuawa na wengine zaidi ya 200 walijeruhiwa katika moja ya shambulio baya zaidi la kigaidi kuwahi kutekelezwa nchini humo.

Kundi la Al Qaeda menye uhusiano na wanamgambo wa Al Shabaab, limekiri kuhusika likisema wapiganaji wake walilenga ofisi za wizara ya elimu.

Shambulio hili tayari limekashifiwa na jumuiya ya kimataifa zikiwemo nchi washirika.

Wakati huu umoja wa Afrika ukipanga kupunguza wanajeshi wake nchini Somalia, hofu ya kurejea kwa kundi la Al Shabaab kwenye miji mikubwa inazidi kutanda, huku vikosi vya nchi vikiwa bado havina uwezo wa kukabiliana na wapiganaji hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.