Pata taarifa kuu

Marekani yawekea vikwazo mtandao wa magendo ya silaha nchini Somalia

Marekani imeweka vikwazo Jumanne ikilenga mtandao wa magendo ya silaha unaosambaza silaha kwa kundi la Al Shabab nchini Somalia, siku mbili baada ya shambulio lililodaiwa na kundi hili lenye itikadi kali na kusababisha vifo vya watu 116 katika mji mkuu wa Mogadishu, ikiwa ni shambulio baya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka mitano.

Moshi mweusi kutokana na milipuko ya mabomu mawili katika afisi za Wizara ya Elimu ya Somalia mjini Mogadishu tarehe 29 Oktoba 2022. Picha iliyopatikana kutoka mitandao ya kijamii.
Moshi mweusi kutokana na milipuko ya mabomu mawili katika afisi za Wizara ya Elimu ya Somalia mjini Mogadishu tarehe 29 Oktoba 2022. Picha iliyopatikana kutoka mitandao ya kijamii. ABDIHALIM BASHIR via REUTERS - ABDIHALIM BASHIR
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Fedha ya Marekani imewaorodhesha watu wanane na kampuni inayohusika na biashara haramu ya silaha kupitia Iran, Yemen na Pembe ya Afrika, na hivyo kuchochea ghasia katika eneo hilo, kulingana na taarifa.

"Watu hawa na taasisi iliyotajwa leo ni vipengele muhimu vya mtandao wa magendo ya silaha ambao umeunganishwa kikamilifu na kundi la Islamic State-Somalia," taarifa ya Wizara ya Fedha ya Marekani imesema.

Mitandao hii inafanya kazi "hasa ​​kati ya Yemen na Somalia na ina uhusiano wa karibu na kundi la wanajihadi la al-Qaeda katika Rasi ya Arabia (Aqpa) na al Shabab".

Wizara ya Fedha ya Marekani hasa imemtaja Abdirahman Mohamed Omar, ambaye anafanya kazi katika eneo la Puntland kaskazini mashariki mwa Somalia, ikimtuhumu kwa kuwapa Waislam wenye itikadi kali silaha zenye thamani ya karibu dola milioni 2 katika kipindi cha miaka minne iliyopita.

Somalia, nchi iliyoko katika Pembe ya Afrika, imetumbukia katika machafuko tangu kuanguka kwa utawala wa Siad Barre mwaka wa 1991. Kundi la wanajihadi wa Al-Shabaab wenye mafungamano na Al-Qaeda wamekuwa wakipambana na serikali ya shirikisho inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa tangu mwaka 2007.

Vikwazo vya Marekani vina athari ya kuzuia mali yoyote ya watu hawa chini ya mamlaka ya Marekani na kupiga marufuku biashara yoyote ya makampuni ya Marekani au watu binafsi na watu hawa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.