Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Somalia: Tisa waangamia katika milipuko ya mabomu mawili katika Wizara ya Elimu

Nchini Somalia, magari mawili yaliyokuwa na mabomu yamelipuka kwenye afisi ya Wizara ya Elimu ya Somalia Jumamosi hii, Oktoba 29, huko Mogadishu.  

Moshi kutokana na milipuko ya mabomu mawili ya gari kwenye afisi ya Wizara ya Elimu ya Somalia mjini Mogadishu tarehe 29 Oktoba 2022. Picha iliyopatikana kupitia mitandao ya kijamii.
Moshi kutokana na milipuko ya mabomu mawili ya gari kwenye afisi ya Wizara ya Elimu ya Somalia mjini Mogadishu tarehe 29 Oktoba 2022. Picha iliyopatikana kupitia mitandao ya kijamii. ABDIHALIM BASHIR via REUTERS - ABDIHALIM BASHIR
Matangazo ya kibiashara

"Milipuko miwili ya wakati mmoja" imetokea kwenye barabara kando ya wizara na kusababisha "vifo kadhaa", msemaji wa polisi ya Somalia Sadik Dudishe amesema, na kuongeza: "Tutatoa maelezo zaidi baadaye. Shambulio hili la mabomu mawili liliua takriban watu tisa, kulingana na vyanzo vya usalama.

Shambulio hilo lilitokea mchana na moja ya milipuko hiyo inaripotiwa kukumba afisi za Wizara ya Elimu.

Hadi kufikia sasa, hakuna taarifa zozote zilizotolewa zinazoangazia idadi ya watu waliojeruhiwa wala hakuna aliyedai kuhusika na milipuko hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.