Pata taarifa kuu

Somalia: Sura mpya zajitokeza dhidi ya Al Shabab, miaka 5 baada ya shambulio la Mogadishu

Ijumaa, Oktoba 14 uliadhimishwa mwaka wa tano wa shambulio baya zaidi la kigaidi barani Afrika. Watu elfu moja waliuawa au kujeruhiwa katika shambulio la bomu la kujitoa muhanga katika lori mjini Mogadishu, shambulio lililohusishwa na kundi la wanajihadi la Al Shabab. Miaka mitano baadaye, mapambano dhidi ya kundi hili lenye silaha nchini Somalia na vikosi vya Umoja wa Afrika yalibadilisha mkakati hivi karibuni, baada ya kuchaguliwa kwa rais mpya kuongoza serikali ya shirikisho.

Familia zinaomboleza ndugu zao waliouawa katika shambulio la bomu lililotegwa katika lori mjini Mogadishu mnamo Oktoba 14, 2017, ambalo liliua watu elfu moja na wengine kujeruhiwa.
Familia zinaomboleza ndugu zao waliouawa katika shambulio la bomu lililotegwa katika lori mjini Mogadishu mnamo Oktoba 14, 2017, ambalo liliua watu elfu moja na wengine kujeruhiwa. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Wanajiita 'Ma'awisley', wavaaji wa 'ma'awis', vazi linaloaliwa na wakulima wa Somalia. Watu hao ni wakulima na watoto wa wakulima, wanaojihami kwa bunduni aina ya Kalashnikov na wakiongozwa na wazee wao. Ni wanamgambo watiifu kwa ukoo wao, maskini kutokana na ukame na kukataa kulipa kodi kwa wanajihadi.

"Vita ya kamili"

Rais wa Somalia Hassan Cheikh Mohamoud aliwafanya wasaidizi wapya wa "vita kamili" ambavyo alitangaza kwa kundi la wanajihadi mnamo Agosti 24. Katika eneo lao la Hiraan, "Ma'awisley" waliwezesha kutwaa vijiji hamsini.

Wakati huo huo, mwezi wa Mei mwaka huu, Mkuu wa Nchi pia aliwaalika Wamarekani, hasa vikosi vyao maalum, kurudi Somalia - ha hata hivyo ndege isiyo na rubani ya Marekani ndiyo iliyomuua Abdullahi Yare, mmoja wa waanzilishi wenza wa kundi la Al Shabab mnamo Oktoba 1 - na mara kwa mara huwahutubia wafanyabiashara na wananchi wa kawaida. Katika hotuba zake rais anawataka kukataa kulipa kodi kwa kundi hilo la kigaidi akibaini kwamba vita hivyo pia vinapaswa kuwa vya kiuchumi.

Walakini, kundi la wanajihadi limejibu vikali - kwa mauaji ya watu waliolengwa, kwa mfano mauaji ya mkuu wa polisi huko Mogadishu mnamo Septemba 30, na kwa mashambulizi, wakati mwingine makubwa, kama huko Beledweyne, Oktoba 3.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.