Pata taarifa kuu

Tisa waawa na makumi ya wengine kujeruhiwa katika shambulio la Al Shabab

Wanamgambo wa Kiislamu wa Al-Shabab walishambulia hoteli moja katika mji wa bandari wa Kismayo, kusini mwa Somalia siku ya Jumapili, na kuua takriban watu tisa na kujeruhi 47.

Al Shabab ilidai kuhusika na shambulio hilo, likidai kulenga hoteli ambayo maafisa wa utawala wa Jubaland walikuwa wakikutana. Mnamo Julai 2019, walifanya shambulio kama hilo dhidi ya viongozi wa eneo hilo katika hoteli moja jijini humo, na kuua watu wasiopungua 26 na kujeruhi 56.
Al Shabab ilidai kuhusika na shambulio hilo, likidai kulenga hoteli ambayo maafisa wa utawala wa Jubaland walikuwa wakikutana. Mnamo Julai 2019, walifanya shambulio kama hilo dhidi ya viongozi wa eneo hilo katika hoteli moja jijini humo, na kuua watu wasiopungua 26 na kujeruhi 56. © AP
Matangazo ya kibiashara

Takriban watu tisa waliuawa na 47 kujeruhiwa katika shambulio lililotekelezwa Jumapili, Oktoba 23 kwa zaidi ya saa sita na wanamgambo wa itikadi kali wa kiislamu wa Al Shabab katika hoteli moja katika mji wa Kismayo, kusini mwa Somalia.

Mji huu mkubwa wa bandari ndio ulioathiriwa hivi karibuni zaidi na kuzuka upya kwa vitendo vya ukatili vilivyofanywa na Al Shabab katika miezi ya hivi karibuni, ambavyo vimesababisha umwagaji damu katika mji mkuu wa Mogadishu na katikati mwa nchi.

Shambulio hilo lililoanza mwendo wa saa 6:45 mchana, lilimalizika mwendo wa saa moja usiku, baada ya washambuliaji watatu waliokuwa ndani ya hoteli hiyo kuuawa kwa kupigwa risasi na vikosi vya usalama vya serikali ya Jubaland.

Waziri wa Usalama wa Jubaland, Yusuf Hussein Osman, alitangaza idadi ya vifo vya watu tisa na wengine 47 kujeruhiwa, "ikiwa ni pamoja na wanafunzi ambao walikuwa wakitoka shule ya karibu wakati wa shambulio hilo". "Vikosi vya usalama vilimaliza operesheni hiyo kwa wakati ufaao," amesema.

Shambulio hilo lilitekelezwa na watu wanne: wa kwanza ambaye alitekeleza shambulio la kujitoa mhanga, na kufuatiwa na uvamizi wa watu watatu waliokuwa na silaha ndani ya hoteli hiyo. Kulingana na Yusuf Hussein Osman, shambulio hilo lilianza na mshambuliaji wa kujitoa mhanga "aliyejilipua".

Al Shabab ilidai kuhusika na shambulio hilo, likidai kulenga hoteli ambayo maafisa wa utawala wa Jubaland walikuwa wakikutana. Mnamo Julai 2019, walifanya shambulio kama hilo dhidi ya viongozi wa eneo hilo katika hoteli moja jijini humo, na kuua watu wasiopungua 26 na kujeruhi 56.

Kundi la Kiislamu lenye uhusiano na Al-Qaeda, limekuwa likipigana na serikali ya shirikisho inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa tangu mwaka 2007.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.