Pata taarifa kuu

Tabia nchi: Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lataka misaada zaidi kwa nchi maskini

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa siku ya Ijumaa limetoa wito wa kuongezwa msaada wa kifedha kwa nchi zinazoendelea ili kukabiliana na mabadiliko ya Tabia nchi, katika azimio la kuunga mkono Pakistan iliyoharibiwa na mafuriko ya kihistoria.

Watu milioni 6.4 nchini Pakistan wanahitaji haraka msaada wa kibinadamu, inaonya WHO.
Watu milioni 6.4 nchini Pakistan wanahitaji haraka msaada wa kibinadamu, inaonya WHO. © AP/Fareed Khan
Matangazo ya kibiashara

Nchi maskini zaidi ndizo zinazokabiliwa zaidi na hatari za mabadiliko ya Tabia nchi na zinahitaji msaada wa kimataifa kufadhili kukabiliana na hali hiyo, kulingana na ripoti ya hivi karibuni na Shirika la Kimataifa la Fedha, IMF.

Nchi zote, ziwe tajiri au maskini, lazima zikabiliane na mabadiliko ya Tabia nchi. Ripoti ya hivi majuzi ya Jopo la kiserikali la Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabia nchi inaweka wazi athari mabaya ikiwa tutashindwa kuzuia ongezeko la joto duniani na kukabiliana na sayari yenye joto zaidi. Marekebisho yanapaswa kushughulikia hatari zinazohusiana na mabadiliko ya Tabia nchi na athari mbaya za hali ya hewa, kwa mfano kwa kulinda kilimo, kudhibiti athari za kupanda kwa maji na kuimarisha miundombinu.

Manufaa ya kukabiliana na hali hiyo wakati mwingine ni ngumu kukadiria, kwani hutegemea vipengele maalum kama vile jinsi nchi inavyozoea hali ya hewa yake ya sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.