Pata taarifa kuu

Pakistan yatangaza hali ya hatari kufuatia mvua kubwa inayonyesha

Mamilioni ya watu wameathiriwa na mafuriko nchini Pakistan tangu kuanza kwa mvua ya masika katikati ya mwezi Juni 2022. Katika baadhi ya majimbo, hadi 780% zaidi ya mvua ilinyesha mwezi huu kuliko wastani wa mwezi wa Agosti mwaka jana. 

Mamia ya vijiji vimemezwa na mvua kubwa iliyonyesha. Zaidi ya nyumba 770,000 zimeharibiwa au kusombwa kote nchini.
Mamia ya vijiji vimemezwa na mvua kubwa iliyonyesha. Zaidi ya nyumba 770,000 zimeharibiwa au kusombwa kote nchini. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Watu katika majimbo ya Balochistan, Khyber Pakhtunkhwa na Sindh ambapo maeneo yaliyoathirika zaidi ni sehemu duni za mashambani, huku mvua ikiendelea kunyesha.

Pakistan inakabiliwa na mafuriko makubwa. Mvua kubwa ambazo zimekuwa zikinyesha tangu katikati ya mwezi wa Juni zimegeuza baadhi ya mito kuwa mafuriko. Mashahidi kadhaa wamerusha video ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii. Katika video hizi kunaonekana hoteli moja ikiporomoka kwa sekunde chache au jengo la kibiashara linalosombwa na maji katika Bonde la Swat, katika jimbo la Khyber Pakhtunkhwa, kaskazini-magharibi mwa nchi. Mkoa huu ndio ulioathirika zaidi na ule wa Balochistan na Sindh.

Mamia ya vijiji vimemezwa na mvua kubwa iliyonyesha. Zaidi ya nyumba 770,000 zimeharibiwa au kusombwa kote nchini. Zaidi ya watu 930 wameuawa katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita, ng'ombe 500,000 wamekufa, mamia ya hekta za mazao zimesombwa na maji. Mafuriko ya ghafla yalisababisha maporomoko ya ardhi, uharibifu wa mabwawa. Zaidi ya kilomita 3,000 za barabara ziliharibiwa.

Kipindupindu

Shule 570 zimeharibiwa nchini kote. Maelfu ya walionusurika wamepata makazi mapya katika mahema ya muda kando ya barabara na kuishi kwao kunategemea michango ya chakula. Aidha, visa vya kipindupindu vimeripotiwa.

Kulingana na mamlaka, mafuriko yaliyoikumba nchi hii yanalinganishwa na yale ya mwaka wa 2010. Watu elfu mbili waliuawa na karibu theluthi moja ya nchi ilisomwa na mvua. Kipindi cha Masika huanza katikati yamwezi Juni na hudumu hadi mwezi Septemba nchini Pakistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.