Pata taarifa kuu
PAKISTAN-SIASA

Pakistani: Rais avunja Baraza la Wawakilishi

Rais wa Pakistan, Arif Alvi, ametangaza siku ya Jumapili kuvunjwa kwa Bunge la Kitaifa. Uamuzi huu unakuja baada ya ombi la Waziri Mkuu Imran Khan na kuzuiwa kwa kura ya hoja ya kutokuwa na imani dhidi yake.

Vikosi vya usalama vinasimama nje ya jengo la bunge huko Islamabad mnamo Aprili 3, 2022.
Vikosi vya usalama vinasimama nje ya jengo la bunge huko Islamabad mnamo Aprili 3, 2022. AFP - AAMIR QURESHI
Matangazo ya kibiashara

Bunge la Kitaifa la Pakistan limevunjwa siku ya Jumapili na Rais Arif Alvi. "Rais wa Pakistan, Dkt. Arif Alvi, ameidhinisha ombi la Waziri Mkuu," ofisi ya rais imesema katika taarifa. Kuvunjwa huku kutapelekea kuitishwa kwa uchaguzi wa mapema wa wabunge katika kipindi cha siku 90.

Waziri wa Habari Fawad Chaudhry pia amebaini kwenye Twitter kwamba Waziri Mkuu amewasilisha kujiuzulu kwa serikali yake na kwamba atashughulikia mambo ya sasa hadi uchaguzi ufanyike, kwa mujibu wa masharti ya Katiba.

Kura ya kutokuwa na imani yazuiwa

Saa chache mapema, Waziri Mkuu Imran Khan alikuwa amemtaka mkuu wa nchi kuchukua madaraka baada ya kunusurika kura ya kutokuwa na imani. "Tutakata rufaa kwa umma, tutafanya uchaguzi na kuacha taifa liamue," amesema wakati wa hotuba kwenye televisheni ya taifa.

Kura ya kutokuwa na imani dhi ya waziri mkuu ilizinduliwa na wapinzani wake wakimtuhumu kwa usimamizi mbovu wa uchumi na uzembe katika sera za kigeni, hoja hiyo hata hivyo haikupigiwa kura. Mara tu kikao cha bunge kilipofunguliwa, makamu wa Spika wa Bunge la Kitaifa, Qasim Suri, mwaminifu wa Bw. Khan, alitangaza kwamba alikataa kuzingatia hoja ya kutokuwa na imani. Aliona kuwa ni “kinyume cha katiba” na kuchochewa na “mamlaka ya kigeni”, hivyo akitumia hoja zile zile za Waziri Mkuu. Uamuzi huu ulizua taharuki miongoni mwa wabunge.

Waziri Mkuu alikuwa kiini cha mzozo wa kisiasa kwa wiki kadhaa. wabunge wengi kutoka kambi yake walikuwa wameamua hata hivyo kujiunga na upinzani, na kusababisha apoteze wingi wa wabunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.