Pata taarifa kuu
IRAN-USALAMA

Iran: Mvutano wazuka kwenye mipaka ya mashariki na Pakistan na Afghanistan

Kulingana na mamlaka, mapigano kati ya vikosi vya Walinzi wa Mapinduzi na "majambazi wenye silaha" yametokea katika mkoa wa Sistan-Balochistan, ulio kwenye mpaka na Pakistan. Watu sita kutoka kundi hili la "majambazi" na askari watatu wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi katika eneo hilo wameuawa.

Wanajeshi wa Iran wakiwa katika mazoezi ya kijeshi katika mkoa wa Sistan na Balochistan, kwenye mpaka na Pakistan.
Wanajeshi wa Iran wakiwa katika mazoezi ya kijeshi katika mkoa wa Sistan na Balochistan, kwenye mpaka na Pakistan. AFP PHOTO/FARSNEWS/STR
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi, mapigano haya makali yalitokea wakati wa shambulio la kushtukiza kwenye maficho ya kikundi cha majambazi kinachoongozwa na Gholam Shahbaksh, ambaye ameuawa wakati wa operesheni hii. Wiki moja iliyopita, watu watano wakiwemo askari wawili wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi waliuawa katika mapigano na watu wenye silaha kutoka kundi hilo lenye silaha.

Jimbo la Sistan-Baluchistan, ambalo lina Wasunni wengi walio wachache, mara kwa mara huwa eneo la mapigano ya silaha kati ya polisi na walanguzi wa dawa za kulevya au makundi ya wanaotaka kujitenga ya Balouche au wanajihadi.

Mvutano wa silaha kwenye mipaka ya mashariki ya Iran

Tehran iliishutumu Pakistan siku za nyuma kwa kuunga mkono makundi yanayotaka kujitenga au kuwaruhusu kufanya shughuli zao kutoka eneo la Pakistan. Jimbo la Sistan Balouchistan linapakana na Pakistan lakini pia Afghanistan ambako Taliban wamechukua mamlaka.

Wiki chache zilizopita mapigano yaliripotiwa kati ya kundi la Taliban na vikosi vya usalama vya Iran bila kusababisha hasara yoyote. Baadhi ya wataalam wanahofia kwamba Taliban, ambao ni Wasunni wenye itikadi kali, watasaidia makundi ya Iran yanayotaka kujitenga yanayoendesha shughuli zake katika eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.