Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Ufaransa yalaani kitendo cha Iran cha kurusha roketi angani

Katika taarifa iliyotolewa Ijumaa, Wizara ya Mambo ya Nje inakashifu tabia ya Iran, ambayo inasema inakiuka "azimio 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa".

Roketi ya kubeba satelaiti ya Iran "Simorgh" yarushwa katika eneo lisilojulikana nchini Iran. Hii ni picha iliyotolewa Desemba 30, 2021.
Roketi ya kubeba satelaiti ya Iran "Simorgh" yarushwa katika eneo lisilojulikana nchini Iran. Hii ni picha iliyotolewa Desemba 30, 2021. via REUTERS - WANA NEWS AGENCY
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa "imeshutumu" Ijumaa, Desemba 31, kitendo cha Iran cha kurusha roketi angani siku siku ya Alhamisi wakati mazungumzo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran yalianza tena. "Ufaransa inalaani uzinduzi huu ambao hauambatani na azimio 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa", diplomasia ya Ufaransa imebainisha katika taarifa kwa vyombo vya habari. "Shughuli hizi ni za kusikitisha zaidi kwani zinakuja wakati tunapiga hatua katika mazungumzo ya nyuklia huko Vienna."

Iran ilisema Alhamisi kuwa ilirusha roketi iliyokuwa imebeba vifaa vitatu vya utafiti angani. "Kutokana na ukaribu wa teknolojia zinazotumiwa kwa kurusha vyombo vya angani na makomboya ya masafa marefu , uzinduzi huu unachangia moja kwa moja katika maendeleo ya Iran ambayo tayari yanatia wasiwasi katika mpango wake wa makombora ya masafa marefu. Jukumu la Wizara ya Ulinzi katika kurusha makombora haya ni ushahidi wa uhusiano wa karibu kati ya mambo haya mawili", imebaini Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa, Quai d'Orsay.

Mazungumzo yanaendelea kuokoa Mkataba wa Vienna

"Uzinduzi huu pia unafuatia kurushwa kwa makombora ya masafa marefu mnamo Desemba 24", pia sio kwa mujibu wa azimio 2231 ambalo "linatoa wito kwa Iran kutofanya shughuli zinazohusiana na makombora ya masafa marefu iliyoundwa kuwa na uwezo wa kubeba silaha za nyuklia ", imesema Wizara ya mambo ya Nje ya Ufaransa. "Programu ya makombora ya masafa marefu ya Iran ni chanzo cha wasiwasi kwa jumuiya ya kimataifa", inaongeza taarifa hiyo ambayo inaitaka Iran "kuheshimu wajibu wake (...), ikiwa ni pamoja na yale yanayohusu uhamisho wa silaha na teknolojia nyeti" .

Urushwaji wa roketi unakuja katikati ya mazungumzo ya kuokoa Mkataba wa Vienna. Mazungumzo hayo yalizinduliwa tena mwishoni mwa mwezi Novemba, baada ya kusimama kwa miezi mitano, kati ya Tehran na nchi ambazo bado zinashiriki katika makubaliano hayo (Ufaransa, Uingereza, Ujerumani, Urusi, Uchina).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.