Pata taarifa kuu
IRAN-USHIRIKIANO

Nyuklia: Iran ‘yaazimia’ kupata mkataba Vienna

Huku mazungumzo yakianza tena mjini Vienna Jumatatu hii, Novemba 29, Iran imetangaza kwamba "imeazimia kithabiti" kufikia makubaliano na jumuiya ya kimataifa kuhusu suala la nyuklia, ametangaza msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran.

Bendera ya Iran ikipepea mbele ya makao makuu ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) huko Vienna, Austria Mei 23, 2021.
Bendera ya Iran ikipepea mbele ya makao makuu ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) huko Vienna, Austria Mei 23, 2021. © REUTERS/Leonhard Foeger//File Photo
Matangazo ya kibiashara

"Ujumbe wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran uko Vienna ukiwa na dhamira thabiti ya kufikia makubaliano na unatarajia mazungumzo yenye tija," Saïd Khatibzadeh amewaambia waandishi wa habari. “Serikali imeonyesha nia yake na umakini wake kwa kutuma timu yenye ubora inayojulikana kwa wote. Ikiwa upande mwingine utaonyesha nia njema, tutakuwa kwenye njia sahihi kufikia makubaliano, "ameongeza.

Marekani kushiriki mazungumzo kwa njia isiyo ya moja kwa moja katika majadiliano

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran, ujumbe wa Iran unaoongozwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Ali Bagheri uko sawa kwa ajili ya duru hii mpya ya mazungumzo. "Ikiwa Marekani itakuja Vienna kwa dhamira ya kuondokana na mkwamo huu na kuondokana na matatizo ambayo hatukukubaliana katika duru zilizopita, njia ya mazungumzo bila shaka itakuwa rahisi," amebaini msemaji huyo.

Mazungumzo ya nyuklia ya Iran yaliyositishwa tangu mwezi Juni, yataanza tena kati ya Tehran kwa upande mmoja na nchi ambazo bado ni sehemu ya makubaliano yaliyohitimishwa mnamo mwaka 2015, ambayo ni Ujerumani, China, Ufaransa, Uingereza na Urusi. Marekani, ambayo ilijitoa kwenye mkataba huo mwaka 2018 chini ya utawala wa rais Donald Trump na kurejesha vikwazo dhidi ya Iran, itashiriki kwa njia isiyo ya moja kwa moja katika majadiliano.

mkataba huo, unayojulikana kwa kifupi kwa lugha ya Kiingereza kama JCPOA, unaipa Tehran kuondolewa kwa sehemu ya vikwazo vinavyodhoofisha uchumi, huku ikitakiwa kupunguza mpango wake wa nyuklia, uliyowekwa chini ya udhibiti mkali wa Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.