Pata taarifa kuu
IRAN-USHIRIKIANO

Nyuklia: Iran yakubaliana na IAEA kubadili kamera zilizoharibika Karaj

Iran na shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) wamekubaliana kubadili kamera za uchunguzi zilizoharibika katika eneo la Tessa huko Karaj, ambapo Tehran inazalisha mashinepewa (centrifuges) za kisasa za nyuklia.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Rafael Grossi na Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran Mohammad Eslami wakati wa mkutano wao mjini Tehran tarehe 23 Novemba 2021.
Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) Rafael Grossi na Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran Mohammad Eslami wakati wa mkutano wao mjini Tehran tarehe 23 Novemba 2021. © Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ya kukaribishwa kwa upande wa Iran inajiri wakati mazungumzo na mataifa yenye nguvu kubwa  huko mjini Vienna hayajapiga hatua yoyote kufufua makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015.

Tehran ilifutilia mbali ombi la shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) la kubadilisha kamera hizo zilizoharibika baada ya kitendo cha hujuma mwezi Juni mwaka jana kilichohusishwa na Iran na Israel.

Iran inatengeneza mashinepewa (centrifuges) za kisasa kwenye eneo hili ambazo hutumika kurutubisha uranium. Hatima ya centrifuges hizi ni mojawapo ya pointi za kutokubaliana katika mazungumzo ya Vienna. mashinepewa  hizi zina nguvu zaidi na kuwezesha Iran kuharakisha urutubishaji wa uranium.

Kulingana na makubaliano ya mwaka 2015, Tehran lazima ipunguze urutubishaji wake hadi chini ya 4%.

Iwapo Iran itakubali kuwa shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA) libadilishe kamera, kwa upande mwingine nchi hiyo itazihifadhi video hizo na haitazipa IAEA hadi makubaliano yamefikiwa mjini Vienna.

Mazungumzo haya kwa sasa yamekwama, juu ya kuondolewa kwa vikwazo na Wamarekani, lakini pia hatua ambazo Tehran inapaswa kuchukua ili kupunguza tena mpango wake wa nyuklia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.