Pata taarifa kuu

Pakistan: Makumi ya watu wauawa katika shambulio la bomu katika msikiti wa Peshawar

Shambulio la bomu la kujitoa mhanga katika msikiti wa Kishia huko Peshawar, kaskazini-magharibi mwa Pakistan, wakati wa sala ya Ijumaa, limesababisha vifo vya watu 56 na karibu 200 kujeruhiwa.

Katika msikiti huu wa Peshawar ndipo kulitokea shambulio la kujitoa mhanga lililoua makumi ya wauumini wa Kishia Ijumaa Machi 4, 2022.
Katika msikiti huu wa Peshawar ndipo kulitokea shambulio la kujitoa mhanga lililoua makumi ya wauumini wa Kishia Ijumaa Machi 4, 2022. REUTERS - FAYAZ AZIZ
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo ulitokea dakika chache kabla ya kuanza kwa sala  Ijumaa hii Machi 4. Msikiti huo wanakoabudia Washia, uko kwenye barabara ndogo katika wilaya ya Kocha Risaldar.

 

“Nilikuwa nje kidogo ya msikiti nilipomuona mwanamume akiwapiga risasi polisi wawili kabla ya kuingia msikitini. Sekunde chache baadaye, nilisikia kishindo kikubwa,” shuhuda Zahid Khan ameliambia shirika la habari la AFP.

Muhammad Ali Seif, msemaji wa serikali ya mkoa wa Khyber Pakhtunkhwa, ambao Peshawar ndio mji mkuu wake, amethibitisha vifo vya watu wengi waliokufa na kujeruhiwa. "Lilikuwa ni shambulio la kujitoa mhanga," amesema pia. Idadi vifo inaweza kuongezeka.

Mji huo unaopatikana takriban kilomita hamsini kutoka mpaka na Afghanistan, ulikuwa umekumbwa na mashambulizi karibu ya kila siku katika nusu ya kwanza ya miaka ya 2010, lakini usalama ulikuwa umeimarishwa sana huko katika miaka ya hivi karibuni. Shambulio la mwisho la ukubwa kama huo lilitokea mnamo mwezi wa Novemba 2018, wakati watu wasiopungua 31 waliuawa katika shambulio la kujitolea mhanga katika soko la jiji.

Lakini kwa wiki chache zilizopita, nchi hiyo imekuwa ikikabiliwa na kurejea kwa nguvu kwa Tehreek-e-Taliban Pakistan (TTP), Taliban ya Pakistani, hali iliyosababishwa na kuingia kwa Taliban madarakani mwezi Agosti nchini Afghanistan. Vuguvugu hili, tofauti na lile la viongozi wapya wa Afghanistan lakini ambalo lina linatoka sehemu mmoja, limedai kuhusika na mashambulizi kadhaa tangu mwanzoni mwa mwaka huu, likiwemo lile lililotekelezwa dhidi ya kito cha ukaguzi cha polisi mjini Islamabad, ambapo polisi mmoja aliuawa na wawili kujeruhiwa. .

Washia nchini Pakistan pia wamekuwa wakilengwa na kundi la Islamic State hapo awali. Tawi lake la kikanda, Islamic State-Khorasan (EI-K), limedai kuhusika na mashambulizi mengi nchini katika miaka ya hivi karibuni, kama vile mauaji ya mapema 2021 ya watoto kumi wa Hazara, kabila la Kishia, katika jimbo la Balochistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.