Pata taarifa kuu
PAKISTAN-SIASA

Pakistan: Mvutano waibuka kati ya jeshi na Imran Khan juu ya uteuzi wa mkuu wa ujasusi

Mgogoro umeibuka kati ya kiongozi wa serikali wa Pakistan Imran Khan na idara ya ujasusi wa jeshi la Pakistani, kuhusu uteuzi wa mkurugenzi mpya wa idara ya ujasusi wa jeshi (ISI).

Mgogoro umeibuka kati ya kiongozi wa serikali wa Pakistan Imran Khan na idara ya ujasusi wa jeshi la Pakistani, kuhusu uteuzi wa mkurugenzi mpya wa idara ya ujasusi wa jeshi (ISI).
Mgogoro umeibuka kati ya kiongozi wa serikali wa Pakistan Imran Khan na idara ya ujasusi wa jeshi la Pakistani, kuhusu uteuzi wa mkurugenzi mpya wa idara ya ujasusi wa jeshi (ISI). AP - B.K. Bangash
Matangazo ya kibiashara

Idara ya ujasusi wa jeshi la Pakistani (ISI) ilitangaza jina la mkurugenzi mkuu wao mpya mnamo Oktoba 6. Luteni Jenerali Nadeem Anjum aliteuliwa kuchukua nafasi ya Jenerali Faiz Hameed kama mkuu wa idara ya ujasusi wa jeshi. Isipokuwa uteuzi huu haukufuata hatua za kawaida.

Kawaida, mkuu wa jeshi anawasilisha orodha ya majina matatu ya majenerali kwa waziri mkuu, ambaye huchagua kutoka kwa maafisa wakuu watatu wa jeshi yule ambaye ataongoza ISI. Huu ni mchakato ambao unategemea sheria za jadi na sio sheria za nchi, kwani hakuna sheria ya kijadi inayotoa uteuzi wa mkuu wa idara kubwa zaidi ya ujasusi ya Pakistan.

Mvutano waongezeka

Imran Khan ameapa kukabiliana na uteuzi huo. Anadai kuwa na neno la mwisho kwa uteuzi wa mkuu wa idara ya ujasusi ya Pakistan.

Kwa mvutano huu kuhusu uteuzi wa mkuu mpya wa ISI, ni mzozo mkubwa kati ya viongozi wa kisiasa na jeshi unaoibuka, kulingana na wachambuzi kadhaa wa kisiasa. Pande hizo mbili kwa sasa zimetofautiana kabisa. Mvutano pia hujumuisha masuala mengine kama sera ya kigeni na usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.