Pata taarifa kuu
PAKISTANI-USALAMA

Angalau watu 13 wauawa na mlipuko wa bomu kaskazini mwa Pakistan

Takriban watu 13, wakiwemo raia tisa wa China na wanajeshi wawili wa Pakistani, wameuawa Jumatano wiki hii katika mlipuko wa bomu lililolenga basi lao kaskazini mwa Pakistan, vyanzo kadhaa vimesema. Idadi hiyo inaweza kuongezeka.

Ni vigumu kusema ikiwa mlipuko huo ulisababishwa na kifaa cha kulipuka kilichowekwa ndani ya basi au kando ya barabara.
Ni vigumu kusema ikiwa mlipuko huo ulisababishwa na kifaa cha kulipuka kilichowekwa ndani ya basi au kando ya barabara. AP
Matangazo ya kibiashara

Moazzam Jah Ansari, mkuu wa Polisi huko Khyber-Paktunkhwa, mkoa ambao tukio hilo limetokea, amethibitisha vifo vya raia sita wa China, wanajeshi wawili na raia wawili.

"Basi lilitumbukia kwenye bonde baada ya mlipuko na kusababisha majeruhi makubwa. Mhandisi wa China na mwanajeshi mmoja wamekosekana. Operesheni ya uokoaji imezinduliwa na serikali imetuma timu zake katika shughuli ya kuwaokoa waliojeruhiwa na gari la wagonjwa", afisa mwandamizi nchini humo ameliambia shirika la habari la REUTERS kwa sharti la kutotajwa jina.

Ni vigumu kusema ikiwa mlipuko huo ulisababishwa na kifaa cha kulipuka kilichowekwa ndani ya basi au kando ya barabara.

Afisa mwandamizi wa polisi ameliambia shirika la habari la REUTERS kwamba idadi ya vifo imeongezeka hadi 13, wakiwemo raia tisa wa China na wanajeshi wawili.

Kulingana na afisa mwingine, basi hilo lilikuwa limewasafirisha wahandisi 30 wa China kwenye eneo la bwawa la Dasu huko Kohistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.