Pata taarifa kuu
PAKISTANI

Mlipuko dhidi ya hoteli ya kifahari waua wanne Pakistan

Watu wanne wameuawa katika mlipuko wa bomu lililotegwa katika gari kwenye eneo kunakoegeshwa magari katika hoteli ya kifahari kusini magharibi mwa Pakistan Jumatano jioni limesababisha vifo vya watu wanne na 11 kujeruhiwa, viongozi wamesema.

Afisa wa polisi anajibu baada ya mlipuko katika hoteli ya kifahari huko Quetta, Pakistan Aprili 21, 2021.
Afisa wa polisi anajibu baada ya mlipuko katika hoteli ya kifahari huko Quetta, Pakistan Aprili 21, 2021. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Balozi wa China nchini Pakistan alikuwa katika hoteli hiyo lakini hakuwa katika jengo hilo wakati mlipuko huo ulitokea, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Pakistan Sheik Rashid Ahmed amesema.

Afisa wa polisi wa eneo hilo ameliambia shirika la habari la REUTERS kuwa mlipuko "uliathiri vibaya eneo kunakoegeshwa magari katika Hoteli ya Serena". Nasir Malik ameongeza kuwa watu 11 wamejeruhiwa.

Kundi la Taliban nchini Pakistan limedai kuhusika na shambulio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.