Pata taarifa kuu
PAKISTANI-CORONA-AFYA

Coronavirus: Pakistani kuanza kulegeza vizuizi vya kudhibiti Corona Jumamosi Mei 9

Marufuku ya raia kutotoka nje iliyowekwa na serikali nchini Pakistani wiki tano zilizopita ili kujaribu kudhibiti maambukizi ya virusi vya ugonjwa wa Covid-19 itaondolewa Jumamosi Mei 9, licha ya kuongezeka kwa idadi ya visa vya maambukizi nchini, Waziri Mkuu Imran Khan amesema.

Tangu kuanza kwa janga la Corona, watu 24,073 wameambukizwa virusi vya Corona nchini Pakistan, ambapo watu wengine 564 wamefariki dunia
Tangu kuanza kwa janga la Corona, watu 24,073 wameambukizwa virusi vya Corona nchini Pakistan, ambapo watu wengine 564 wamefariki dunia REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Tunaamua kusitisha marufuku ya raia kubaki nyumbani," amesema kwenye televisheni. "Tunajua tunafanya wakati hali inakuwa nzuri (...) lakini ugonjwa wa Covid-19 umeanza kupunguza kasi."

Uamuzi huu umechukuliwa kwa sababu watu wengi nchini, kiuchumi, hawawezi kuendelea kukaa nyumbani na wasifanyi kazi, Waziri Mkuu Imran Khan amebaini.

Tangu kuanza kwa janga la Corona, watu 24,073 wameambukizwa virusi vya Corona nchini Pakistani, ambapo watu wengine 564 wamefariki dunia. Leo Alhamisi, idadi ya kila siku ya visa vipya vya maambukizi imefikia watu 1,523.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.