Pata taarifa kuu
PAKISTANI-USALAMA

Pakistan: Thelathini waangamia katika ajali ya treni karibu na Daharki

Takriban watu 30 wamefariki dunia na makumi kujeruhiwa katika ajali ya treni kusini mwa Pakistan Jumatatu hii, polisi imesema. Shughuli ya uokoaji inaendelea polisi imeongeza.

Shughuli ya uokoaji inaendelea katika eneo la ajali, ambapo treni mbili zimegongana.
Shughuli ya uokoaji inaendelea katika eneo la ajali, ambapo treni mbili zimegongana. REUTERS - STINGER
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na afisa wa shirika la reli nchini Pakistan, treni hiyo ambayo ilikuwa imefika kutoka Karachi iliaacha njia karibu na eneo la Daharki, kaskazini mwa mkoa wa Sindh, kabla ya kugongana uso kwa uso na treni nyingine.

Umar Tufail, afisa wa polisi katika eneo la Daharki, ameripoti idadi ya awali ya vifo 30 katika ajali hiyo.

Treni hiyo iliyo acha njia ya Millat Express inafanya safari kati ya bandari kubwa ya Karachi na Sargodha.

"Watu kadhaa wamefariki dunia na wengine wengi bado wamenakwama ndani ya treni," afisa wa shirika la

reli wa chini Pakistan ameliambia shirika la habari la AFP, akiongeza kuwa shughuli ya uokoaji inaendelea.

Picha za moja kwa moja kutoka kwa simu za rununu zinaonyesha machafu ya chuma na magari kadhaa ya Reli ya Pakistan yaliyopinduliwa.

Ajali za reli hutokea mara nyingi nchini Pakistan, ambayo ina maelfu ya kilomita ya njia na treni kutoka enzi za ukoloni chini ya Dola ya Uingereza.

Lakini sekta hii inakabiliwa na miongo kadhaa ya kutelekezwa kwa sababu ya ufisadi, usimamizi mbaya na ukosefu wa uwekezaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.