Pata taarifa kuu
PAKISTANI

Diplomasia: Pakistan na India washutumiana kwa msimamo mkali

Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan ameshtumu India katika hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa Ijumaa (Septemba 24) kwa "kuchochea vitisho" dhidi ya Waislamu, tuhuma ambzo zimesababisha kuibuka kwa vita vya maneneo kati ya marais wa nchi hizo mbili.

Katika ujumbe wa video, Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan hapo awali alishtumu serikali ya Narendra Modi kwa ufashisti, pamoja na kukemea ukiukaji wa haki za binadamu katika mkoa unaozozaniwa wa Kashmir
Katika ujumbe wa video, Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan hapo awali alishtumu serikali ya Narendra Modi kwa ufashisti, pamoja na kukemea ukiukaji wa haki za binadamu katika mkoa unaozozaniwa wa Kashmir PETER FOLEY POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake kwa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Umoja wa Mataifa, Imran Khan alimshtumu Waziri Mkuu wa India Narendra Modi kwa kutaka "kuitenga India dhidi ya Waislamu" nchini humo.

Diplomasia ya India iliishutumu Pakistan kwa kuunga mkono magaidi na kuwatesa jamii ya watu wachache ambao si Waislamu.

Zaidi ya miaka 70 baada ya uhuru wao, India na Pakistan kwa mara nyingine wameanzisha uhasama wao mbele ya hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa. Kupitia mwanadiplomasia wake Sneha Dubey, India imetoa tuhuma kali dhidi ya jirani yake Pakistan, kwenye hadhara kuu ya Umoja wa Mataifa.

"Mauaji ya kimbari ya kitamaduni na kidini"

"Tunaendelea kusikia kwamba Pakistan ni mwathirika wa ugaidi," Sneha Dubey alisema. Kwa kweli, inawahifadhi magaidi kwa matumaini kwamba watafanya mashambulizi dhidi ya majirani zake. Nchi hii imefanya mauaji ya kitamaduni na kidini dhidi ya watu wa Bangladesh hapo zamani. Leo inawadhalilisha watu kutoka jamii ya Sikh, Hindu na Wakristo wachache. "

Katika ujumbe wa video, Waziri Mkuu wa Pakistan Imran Khan hapo awali alishtumu serikali ya Narendra Modi kwa ufashisti, pamoja na kukemea ukiukaji wa haki za binadamu katika mkoa unaozozaniwa wa Kashmir. Wakati huo India ilijibu ikisema: "Kashmir daima itakuwa sehemu isiyoweza kutengwa ya eneo la India. Tunatoa wito kwa Pakistan kuondoka mara moja katika maeneo yote ambayo inakalia kinyume cha sheria. "

Mvutano unakua

Tangu Taliban ilipochukua madaraka nchini Afghanistan, mzozo umekuwa ukiongezeka kati ya nchi hizo mbili. India inashtumu Pakistan kwa kutumika kama ngome kuu na hifadhi kwa Taliban. Jumamosi hii, Septemba 25, Imran Khan amebaini kwa upande wake kwamba mazungumzo na Taliban ndiyo ilikuwa suluhisho pekee.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.