Pata taarifa kuu

Mafuriko nchini Pakistan: Waziri Mkuu Sharif aonya nchi zinazochafua mazingira

Nchini Pakistan, mafuriko yamekumba theluthi moja ya nchi na kusababisha vifo vya karibu watu 1,600 tangu mwezi Juni 2022. Wakati viongozi wengi, tangu Jumanne, wamezungumza juu ya mabadiliko ya hali ya hewa kwenye jukwaa la Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, huko New York, nchini Marekani. 

Nchini Pakistan, mafuriko yamekumba theluthi moja ya nchi na kuua karibu watu 1,600 tangu mwezi Juni 2022.
Nchini Pakistan, mafuriko yamekumba theluthi moja ya nchi na kuua karibu watu 1,600 tangu mwezi Juni 2022. AP - Muhammad Sajjad
Matangazo ya kibiashara

Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif alielezea kwa uchungu nchi yake iliyoharibiwa, na akanyooshea kidole cha lawama jukumu kwa nchi zinazochafua mazingira.

Mafuriko 'mabaya' yaliyoikumba Pakistan msimu huu wa kiangazi ni utangulizi tu kwa sayari nzima kuwa inaathiriwa na mabadiliko ya Tabia nchi, Waziri Mkuu wa Pakistani Shehbaz Sharif alionya siku ya Ijumaa, Septemba 23, kwenye jukwaa la mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. "Ninaposimama hapa. , moyo wangu na akili yangu vinaelekezwa katika nchi yangu. Huwa nahisi kama ninatembelea mojawapo ya maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko. Kwa siku arobaini mchana na usiku tumeangukia na gharika. Katika Ground Zero ya mabadiliko ya Tabia nchi, mamilioni ya wahamiaji wa hali ya hewa bado wanatafuta sehemu ndogo ya ardhi, ambako wanaweza kukimbilia, sehemu kavu ili kuweka hema zao, wakiomboleza ndugu zao waliopoteza, wakifikiria maisha yao ya baadaye, riziki zao. »

"Je, tutalazimika kudhibiti mgogoro huu peke yetu"

"Ni wakati wa kujiuliza sio nini kinachoweza kufanyika lakini nini kifanyike," Shehbaz Sharif alisema. Kinachotokea Pakistan hakipaswi tu kuhusisha Pakistan. Maeneo nyeti kama vile nchi yangu yamo kwenye orodha ya nchi kumi zilizo hatarini zaidi na mabadiliko ya Tabia nchi, lakini yanatoa chini ya 1% ya gesi chafu. Kwa hivyo ni busara kutarajia angalau mwonekano wa haki kwa hasara na uharibifu huu. Tunapotoka kwenye mkutano huu wa mwezi Agosti, na tunazungumza juu ya migogoro kama huko Ukraine, swali ninalojiuliza ni je, tutakuwa peke yetu? Itabidi tusimamie mzozo huu peke yetu, tukiachwa kwa hatima yetu, kwa shida ambayo hatukusababisha? "

Theluthi moja ya nchi iko chini ya maji

Mafuriko nchini Pakistan yamesababishwa na mvua kubwa yenye pepo mkali, ambayo nguvu yake inaongezeka kutokana na ongezeko la joto duniani, kulingana na wataalamu na maafisa wa Pakistani, linaandika shirika la habari la AFP. Mafuriko hayo yamefunika theluthi moja ya nchi - eneo lenye ukubwa wa Uingereza - yakiharibu nyumba, biashara, barabara, madaraja na mazao ya kilimo. Akiwa ziarani nchini humo mwezi Septemba, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitangaza kwamba "hajawahi kuona uharibifu wa Tabia nchi wa kiwango hiki", na kutoa wito kwa wachafuzi wakubwa "kukomesha zimwi hili" linalojumuisha kuwekeza zaidi katika nishati ya mafuta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.