Pata taarifa kuu

Pakistan: Idadi ya vifo kutokana na mafuriko makubwa yaongezeka hadi 1,061

Mafuriko yaliyosababishwa na mvua zilizoanza mwezi Juni yameua takriban watu 1,061 nchini Pakistani, kulingana na ripoti ya hivi punde iliyochapishwa Jumatatu, Agosti 29, na Mamlaka ya Kitaifa ya Kukabiliana na Majanga (NDMA), shirika la habari la AFP limeripoti.

Kisima kilichojaa maji kutokana na mafuriko katika eneo la Sukkur (Sind), Agosti 28, 2022.
Kisima kilichojaa maji kutokana na mafuriko katika eneo la Sukkur (Sind), Agosti 28, 2022. AFP - ASIF HASSAN
Matangazo ya kibiashara

Pakistani imekumbwa na mafuriko makubwa kufuatia mvua kubwa ambayo imekuwa ikiikumba nchi hiyo tangu katikati ya Juni 2022. Serikali ilitangaza hali ya hatari Ijumaa Agosti 26 huku mvua ikiendelea kunyesha. Takriban watu 1,061 waliuawa, zaidi ya wakazi milioni 33, au mkazi mmoja kati ya saba, wameathiriwa na mafuriko haya.

Mojawapo ya majimbo yaliyoathirika zaidi ni Sindh kusini mwa nchi. Papo hapo, macho yanaelekezwa kwenye bwawa la Sukkur, kwa sababu ni juu yake kwamba kunategemewa hatima ya mamia ya maelfu ya watu kusini mwa Pakistan. Hifadhi hii ya maji ni msingi wa mfumo wa umwagiliaji nchini Pakistani; pia ni mtandao mkubwa wa umwagiliaji wa aina hii duniani.

Hazina dhaifu ya uhandisi

Ni hazina ya uhandisi ambayo ilianza miaka ya 1930. Inasambaza maji ya Mto Indus katika karibu kilomita 10,000 za mifereji. Milango kumi na tisa ya chuma ya bwawa hili kubwa la mawe ilifunguliwa ili kudhibiti mtiririko wa mto. Kumekuwa tu na uzembe katika matengenezo ya jengo katika miaka ya nyuma na mtiririko wa maji unapunguzwa na tabaka za udongo ambazo zimewekwa kwa muda na ambazo hazijawahi kuondolewa.

90% ya usambazaji wa maji wa Pakistan

Hatari ni kwamba Mto huu Indus, ambao hutoa 90% ya maji nchini Pakistani, hujaa maji na kusababisha mafuriko katika vijiji vyote vinavyozunguka bwawa hilo. Vijiji vingi tayari vimesombwa na maji. Kumeonekana mashamba makubwa ya kilimo, bustani ya miembe na mitende, yakizamishwa chini ya maji na maelfu ya watu walionusurika wakiwa wamekusanyika chini ya mahema ya muda pembezoni mwa barabara.

Waokoaji wana kazi ngumu usiku na mchana kusaidia wakaazi walionaswa lakini pia kuwaletea chakula wale wanaokataa kuondoka makwao licha ya hatari ya kipindi kipya cha mvua kubwa. “Tunaomba mvua zisitishe kunyesha,” wakaazi kadhaa wa Sukkur walituambia, wakitazama anga kwa huzuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.