Pata taarifa kuu

Mafuriko Pakistan: UN yatoa wito wa dharura wa michango ya dola milioni 160

Baada ya mafuriko makubwa ambayo tayari yameua zaidi ya watu 1,136, kulingana na ripoti rasmi ya hivi punde, serikali ya Pakistan ilizindua, Jumanne Agosti 30, kwa pamoja na Umoja wa Mataifa ombi la dharura la michango ya dola milioni 160.

Mwanamke huyu akiwa kati ya kambi ya hema za muda ambapo familia yake imekimbilia, huko Charsadda, Agosti 30, 2022.
Mwanamke huyu akiwa kati ya kambi ya hema za muda ambapo familia yake imekimbilia, huko Charsadda, Agosti 30, 2022. REUTERS - FAYAZ AZIZ
Matangazo ya kibiashara

Jumanne Agosti 30 Pakistan ilizindua ombi la dharura na Umoja wa Mataifa kwa mchango wa dola milioni 160 ili kufadhili mpango wa dharura kwa muda wa miezi sita ijayo, ambayo awali ilikusudiwa kutoa huduma za kimsingi (afya, chakula, maji ya kunywa, makazi) kwa watu Milioni 5.2 walioathirika zaidi.

Pakistan inashukuru nchi zote zinazoifikia ili kukabiliana na athari za mafuriko makubwa. Iwapo juhudi kwa sasa zinalenga misaada ya dharura kwa waathiriwa wa maafa, basi itakuwa muhimu kujenga upya karibu theluthi moja ya nchi iliyoko chini ya maji leo. Zaidi ya watu milioni 33 wameathiriwa na mafuriko haya.

Juhudi kubwa za kifedha wakati nchi hii inapitia mzozo wa kiuchumi, amekumbusha Waziri Mkuu, ambaye amebaini kwamba angalau dola bilioni 10 zinahitajika kukarabati uharibifu huo. "Mafuriko haya ni mabaya zaidi katika historia ya Pakistan," amesema Shehbaz Sharif. Watu hawana makazi, wanahitaji chakula, dawa, maji ya kunywa. Na hali hii mbaya imesababisha hali mbaya ya kiuchumi. Mafuriko haya yametuongezea mzigo. Β»

Mvua hizi zimesomba au kuharib vibaya zaidi ya nyumba milioni moja na kuharibu maeneo makubwa ya ardhi ya kilimo muhimu kwa uchumi. "Ninaahidi kwa dhati kwamba kila senti itatumika kwa uwazi. Kila senti itaenda kwa walengwa,” ameongeza.

Ongezeko la joto duniani

Pakistan inakumbwa na mvua kubwa ya masika baada ya kukumbwa na ukame uliotanguliwa na mawimbi ya kihistoria ya joto mwezi Mei.

Waziri wa Mabadiliko ya Tabianchi Sherry Rehman amesema Pakistan inaathirika pakubwa wakati inazalisha chini ya 1% ya gesi chafu duniani. Hali ya kutisha, ambayo inawezekana kujirudia katika miaka ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.