Pata taarifa kuu
ALGERIA

Algeria: Bouteflika kuzikwa pamoja na mashujaa wa vita vya uhuru

Rais wa zamani wa Algeria Abdelaziz Bouteflika, aliyefariki dunia siku ya Ijumaa, atazikwa Jumapili hii kwenye wa makamburi ya mashujaa ya El Alia huko Algiers, yaliyotengwa kwa mashujaa wa Vita vya Uhuru, lakini hatazikwa kwa heshima zote sawa na watangulizi wake.

Katika maombolezo haya ya siku 3 kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Algeria Abdelaziz Bouteflika,bendera zitapepea kwa nusu mlingoti.
Katika maombolezo haya ya siku 3 kufuatia kifo cha rais wa zamani wa Algeria Abdelaziz Bouteflika,bendera zitapepea kwa nusu mlingoti. AP - Fateh Guidoum
Matangazo ya kibiashara

Bwana Bouteflika, aliyeondolewa mamlakani mnamo mwaka 2019 baada ya kuitawala Algeria kwa miaka 20, alifariki dunia siku ya Ijumaa akiwa na umri wa miaka 84 katika nyumba yake huko Zeralda (magharibi mwa Algiers) ambapo alikuwa akiishi kwa miaka miwili na nusu . Atazikwa baada ya sala ya Dhuhur (baada ya saa 1 mchana saa za Algeria, sawa na saa sita mchana sa za kimataifa), kulingana na televisheni ya serikali.

Mwili wake utapelekwa kwenye makao makuu ya Bunge,katikati mwa Algiers, kuwezesha viongozi mbalimbali serikalini na raia kutoa heshoma za mwisho, kabla ya kuelekea kwenye makaburi ya El Alia, umbali wa kilomita kumi, kulingana na vyombo kadhaa vya habari nchini Algeria.

Ni katika uwanja wa mashahidi wa makaburi haya ambapo watangulizi wake wote walizikwa, ikiwa ni pamoja na watu mashuhuri na mashahidi wa Vita vya Uhuru (1954-1962).

Algeria imetangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa kuanzia jana Jumamosi Septemba 18 2021, kufuatia kifo cha rais wa zamani wa taifa hilo, Abdelaziz Bouteflika.

Ofisi ya rais huyo wa sasa ilisema katika maombolezo hayo ya siku 3 bendera zitapepea kwa nusu mlingoti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.